Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Ongezeko la nauli mzigo kwa Mtanzania’

Muktasari:

  • Kutokana na ongezeko la nauli za daladala na mabasi ya masafa marefu, Mtanzania atalazimika kuongeza bajeti ya usafiri wake kila siku na hivyo kuongeza ugumu wa maisha.

Dar es Salaam. Wakati Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra) ikitangaza ongezeko la nauli za daladala na mabasi ya masafa marefu, imeelezwa kuwa ongezeko hilo litaongeza ugumu wa maisha kwa Watanzania.

Jana Novemba 28, Mkurugenzi wa Latra, Habibu Saluo alitaja miongoni mwa sababu ya kupanda nauli ni pamoja na ongezeko la bei za mafuta na vipuri.

Akiuzungumza katika mjadala wa Mwananchi X-space iliyoendeshwa na Mwananchi Comunications Limited (MCL) ikiwa na mada isemayo ‘Nini maoni yako kuhusu mabadiliko ya nauli ya mabasi’, leo Novemba 29, Mhariri wa takwimu wa Mwananchi, Halili Letea amesema kuna ongezeko kati ya Sh100 hadi Sh300 kwenye nauli hizo kwa safari moja.

“Kwa mtu ambaye nauli yake imeongezeka kwa Sh300 itabidi aongeze bajeti yake kwa mwezi Sh18,000. Kima cha chini cha kipato cha Mtanzania ni Sh300,000, kama atatakiwa kuongeza Sh18,000 kwenye nauli yake  atabaki na Sh282,000 kwa mtu anayeishi peke yake hili ni ongezeko kubwa sana.

Ameongeza, “Kwa ulinganisho wa kima cha chini cha mshahara wa Sh300,000 Mtanzania alikuwa anabaki na Sh270,000 akitumia nauli, lakini ongezekola Sh300 kwenye nauli ya Sh500 sasa atabaki na Sh252,000.”

Hoja hiyo imeungwa mkono na mtumiaji wa usafiri wa ardhini, Glory Olomi aliyeeleza licha ya kupandishwa, huduma zinazotolewa bado ziko chini ya kiwango.

“Kwa sisi tunaosafiri Dar es Salaam Moshi unakuta nauli ya mabasi yamepanda lakini viti kwenye daladala ni vibovu, gari ni chafu huduma ni mbaya. Kwa hiyo nauli unatoa kubwa lakini usafi sio mzuri, unaweza kushika kiti unaenda kuumwa,”amesema

Olomi katika maelezo yake amesisiitiza umuhimu wa kutolewa elimu hasa kwenye mitandao ya jamii ili kuelewa zaidi kiwango kilichopandishwa na jinsi ya kukabiliana ongezeko hilo.

“Kiwango kinachoongezeka kwa mwananchi wa kawaida si kidogo, hivyo tupewe elimu,” amesema

Suala la utoaji wa elimu pia limejadiliwa na mwandishi wa Mwananchi, Fortune Francis aliyesema ni kipindi kifupi cha mabadiliko ya nauli kilichotokana na malalamiko ya wamiliki wa magari kuhusu gharama ya uendeshaji.

“Wananchi nao wamebaki kulalamika, hali inayoonyesha kutokuwepo kwa uelewa wa kutosha,” amesema.

Amesema mabadiliko hayo ni lazima yataathiri sekta nyingine, hivyo ili kumlinda mlaji, ni wajibu wa Tume ya Ushindani (FCC) kutekeleza wajibu wake.