Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Panya Road’ 35 wafikishwa mahakamani, 17 waendelea kuchunguzwa

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla

Muktasari:

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema vijana 35 wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu maarufu ‘Panya Road’ wamefikishwa mahakamani huku uchunguzi wa wengine 17 ukiwa unaendelea.

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema vijana 35 wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu maarufu ‘Panya Road’ wamefikishwa mahakamani huku uchunguzi wa wengine 17 ukiwa unaendelea.

Siku za hivi karibuni kuliibuka matukio ya vijana kufanya vitendo vya kihalifu, ikiwemo kupora na kujeruhi katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

Makalla ameyasema hayo leo Jumatano Mei 18, 2022 wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa uwekaji anuani za makazi Halmashauri ya Temeke.

Amesema Jeshi la Polisi limefanya kazi kubwa kuwa kushirikiana na wenyeviti wa serikali za mitaa, ambao wamehamasisha ulinzi shirikishi.

“Matukio yaliyojitokeza hayatajirudia tena, hawa waliokuwa wamepanga kuvuruga amani kwenye mkoa huu watafute kazi nyingine za kufanya,” amesema Makalla.

Akizungumzia shughuli ya uwekaji anwani za makazi, Makalla amesema ingawa wamefanya vizuri, lakini haikuwa rahisi kwa kuwa kila mmoja alikuwa akisema lake.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nauye amesema shughuli iyo imefikia asilimia 94 huku Mkoa wa Dar es Salaam ukiongoza.

Akizungumza na viongozi wa Halmashauri za Temeke na Kigamboni wakati akikagua utekelezaji wa mradi huo, Nape amesema hadi kufikia Mei 16 ilikuwa umefikia asilimia 94.6 nchi nzima.

Amesema walitakiwa kukabidhi shughuli hiyo Mei 30, na kufikia Mei 16 taatifa za mfumo nchi nzima zimeonyesha kuwa asilimia 94.6 ya wananchi wamefikiwa kwa utambuzi mkoa wa Dar es Salaam ukifanya vizuri kwenye Halmashauri zote," amesema Nape.