Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tatizo la kukatika umeme Dar kumalizika Mei

Muktasari:

  • Akizungumza jana baada ya kutembelea vituo vya Mbagala, Kurasini na Kariakoo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk Tito Mwinuka alisema tatizo hilo linatokana na miundombinu kuzidiwa na watumiaji.

Dar es Salaam. Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), umesema tatizo la kukatika kwa nishati hiyo mara kwa mara jijini hapa litamalizika kabla ya Mei, baada ya ujenzi wa vituo vya kusafirisha na kupooza umeme kukamilika.

Akizungumza jana baada ya kutembelea vituo vya Mbagala, Kurasini na Kariakoo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk Tito Mwinuka alisema tatizo hilo linatokana na miundombinu kuzidiwa na watumiaji.

“Kama mnavyofahamu, Jiji la Dar es Salaam linakua kwa kasi, tunahitaji miundombinu itakayohimili ongezeko kubwa la watu na viwanda,” alisema.

Mwinuka aliyefanya ziara hiyo ya kwanza tangu ateuliwe na Rais John Magufuli mwezi uliopita, alisema kukamilika kwa vituo vya kusafirisha  na kupooza umeme vya Mbagala, Kurasini na Kariakoo, kutamaliza tatizo hilo.