Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Toeni elimu ya kodi kuondoa malalamiko’

Muktasari:

  • Licha ya juhudi zinazochukuliwa na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) kukusanya kodi, imetakiwa kutoa elimu zaidi kwa walipakodi, ili kuondoa malalamiko ya kuona wanaonewa.



Unguja. Licha ya juhudi zinazochukuliwa na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) kukusanya kodi, imetakiwa kutoa elimu zaidi kwa walipakodi, ili kuondoa malalamiko ya kuona wanaonewa.

Imeelezwa wapo walipakodi wanaolalamikia hatua mbalimbali zinazochukuliwa na kuona wananyanyaswa katika ukusanyaji wa kodi, hali inayotajwa inatokana na kuwa na elimu ndogo.

Kauli hiyo ilitolewa na mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi ya Baraza la Wawakilishi, Soud Nahoda Hassan wakati wa majumuisho ya ziara iliyofanyika katika matawi ya ZRB kungalia utendaji kazi wake.

“Licha ya juhudi zinazoendelea kuchukuliwa, elimu bado inahitajika kuona wananchi hawaonewi katika adhabu zinazohusisha masuala ya ulipaji kodi,” alisema.

Hata hivyo, aliwapongeza kwa juhudi za kukusanya kodi na kuwasogezea huduma karibu wananchi hao.

Makusanyo ya kodi ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022/23 (Julai hadi Septemba), ZRB imevuka lengo kwa kukusanya Sh131.7 bilioni kati ya malengo ya kukusanya Sh125.1 bilioni.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Saada Mkuya alisema uamuzi wa kuanzisha vituo vya kodi umelenga kusogeza huduma karibu na walipakodi, ili kurahisisha kukusanya kodi ya Serikali kwenye maeneo hayo na kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari.

Aliwapongeza wafanyabiashara wanaolipa kodi kwa hiari kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na kwamba inaonyesha ufanisi pande zote mbili.