“Watanzania waliomba majina ya watumia ‘unga’ yatajwe hadharani”

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

Muktasari:

Makonda amesema katika uongozi wa Rais Jakaya Kikwete alipigiwa kelele ili awataje wahusika wa dawa za kulevya lakini aliamua kuacha vyombo vyenye mamlaka vifanye kazi yake.

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kutajwa hadharani kwa wahusika wa dawa za kulevya kumetokana na maombi ya Watanzania chini ya uongozi wa awamu ya nne.

Makonda amesema katika uongozi wa Rais Jakaya Kikwete alipigiwa kelele ili awataje wahusika wa dawa za kulevya lakini aliamua kuacha vyombo vyenye mamlaka vifanye kazi yake. 

"Mzee Jakaya mlimpigia kelele...ooh taja taja,  taja taja, sasa tulipoingia sisi tukaona wacha tufanye kama mlivyokuwa mnataka." 

"Wakaibuka tena,  haaa hapana hiyo siyo busara haa...uliona wapi giza linaondolewa kwa kutumia giza? .Aliyefanya mafichoni anawekwa hadharani na harudii tena,"amesema