Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

'Watunzi wa riwaya, mashairi wafunguliwa milango kupelekwa miswada

Meneja Uhusiano na Mawasiliano Mawasiliano wa ALAF Limited (Tanzania) Hawa Bayumi (kulia) akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar sa Salaam kuhusu wito wa kuwasilisha miswada kwa ajili ya Tuzo ya Kiswahili ya Safal ya Fasihi ya Afrika 2024. Kushoto ni Ofisa wa Mawasiliano na Uhusiano Theresia Mmasy.

Muktasari:

  • Mswada ya riwaya lazima iwe baina ya maneno 40,000 hadi 60,000 na kwamba vitabu vilivyokwisha chapishwa havitazingatiwa

Dar es Salaam. Watunzi wa mashairi na riwaya wametakiwa kuwasilisha miswada kwa ajili ya shindano la Tuzo ya Kiswahili ya Safal ya Fasihi ya Afrika la mwaka 2024 linalofanyika kwa msimu wa tisa sasa. Miswada hiyo imeanza kupokewa jana  na shughuli hiyo itandelea mpaka  Novemba 30 2024 itakapofungwa kupisha mchakato utakaowezesha kupatikana washindi.

Imeelezwa kuwa miswada ya riwaya lazima iwe baina ya maneno 40,000 hadi 60,000 na kwamba vitabu vilivyokwisha chapishwa havitazingatiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari, jana Ijumaa Julai 11 2024 Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Alaf Tanzania, Hawa Bayumi amesema ni fahari kubwa kuendeleza udhamini wa tuzo hizo zinazolenga kukuza fasihi na lugha ya Kiswahili kwa jumla.

" Kiswahili ni miongoni mwa lugha zinazokuwa kwa kasi kubwa duniani na kutumika nchi kadhaa Afrika na duniani, hivyo Safal Group ikiwa mzalishaji wa suluhisho bora la ujenzi barani Afrika, hii imekuwa moja ya njia zetu muhimu za kuwajibika kwa jamii. Tunatambua lugha kuwa nyenzo muhimu ya ustawi wa uchumi na jamii, hivyo tutaendelea kuwa wadau muhimu katika kukuza kiswahili," amesema Hawa.

Shindano hilo linadhaminiwa na SafaL Group kupitia kampuni zake tanzu za Alaf Limited (Tanzania) na Mabati Rolling Mills (Kenya).

Safal Group ni mzalishaji na msambazaji mkubwa zaidi wa bidhaa za  ujenzi zenye ubora  barani Afrika katika nchi tisa za Afrika mashariki na kusini.

Hawa amesema  shindano hilo litahusisha miswada ambayo haijachapishwa, katika tanzu za riwaya na ushairi huku zawadi zikiwa na  jumla ni Dola 15,000 za Marekani zitakazotolewa kwa washindi mbalimbali.

Tuzo hizo zilianzishwa mwaka 2014 na Dk Lizzy Attree na Dk Mukoma wa Ngugi ili kutambua uandishi kwa lugha za Kiafrika na pia kuhimiza tafsiri baina ya lugha za Kiafrika zenyewe kwa zenyewe.

Hadi sasa tuzo hizo zimewezesha miswada ya washindi 24 kuchapisha kazi zao katika vitabu kupitia mchapishaji Mkuki na Nyota.

 Kupitia ufadhili wa Safal Group, zaidi ya vitabu 4,000 kutoka kwa waandishi walioshinda vimechapishwa na kusambazwa katika taasisi za kujifunza na maktaba nchini Tanzania na Kenya.

“Wakati juhudi za kuhimiza kusoma na kuandika kwa Kiswahili zinaendelea, tunawahimiza waandishi kutoka Afrika Mashariki na nchi nyengine za Afrika kuwasilisha miswada yao na kushiriki katika shindano la mwaka huu," amesema Hawa.

Mbali na fedha taslimu, miswada itakayoshinda itachapishwa kuwa vitabu na Shirika la Uchapishaji la Mkuki na Nyota (Tanzania), linaloweza kushirikiana na wachapishaji wengine ili kurahisisha upatikanaji wa vitabu vilivyoshinda.

Hawa amesema vitabu vya ushairi vitakavyoshinda vitatafsiriwa kwa Kiingereza na kuchapishwa na Africa Poetry Book Fund.

Tuzo za mwaka 2024 zitatolewa Julai 2025, na waandishi wote walioorodheshwa watahudhuria.

Meneja Uhusiano na Mawasiliano Mawasiliano wa ALAF Limited (Tanzania)   Hawa Bayumi (kulia) akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar sa Salaam kuhusu wito wa kuwasilisha miswada kwa ajili ya Tuzo ya Kiswahili ya Safal ya Fasihi ya Afrika 2024. Kushoto ni Ofisa wa Mawasiliano na Uhusiano Theresia Mmasy.