500 kushiriki Kongamano kujadili uchumi jumuishi kuelekea Dira Maendeleo ya Taifa 2050
Mwenyekiti wa Kongamano la Mgoda na Kigoda cha Mwalimu J.K Nyerere cha Uprofesa kutoka Taaluma ya Umajumui wa Afrika Prof, Alexander Makulilo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kongamano la kujadili Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050. Picha na Hawa Mathias
Muktasari:
- Kongamano hilo limeandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Kituo cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi (PPP Centre),litakalo fanyika kesho Septemba 18, mwaka huu katika Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya.
Mbeya. Wadau wa sekta binafsi, Asasi za kiraia wananchi na viongozi wa Serikali wakiwepo wakuu wa mikoa na Wilaya kushiriki kongamano la kujadili mwenendo wa kiuchumi wa Tanzania kuelekea Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.
Hatua ni kutekeleza maagizo sita yaliyo tolewa na Rais Samia Samia Suluhu Hassan Julai 17, mwaka huu wakati akizindua Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 jijini Dodoma.
Kongamano hilo limeandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP Centre),litakalo fanyika katika Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kongamano na Mgoda wa Kigoda cha Uprofesa wa Mwalimu J.K Nyerere kutoka Taaluma za Umajumui wa Afrika (Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam) Profesa Alexander Makulilo, leo Jumatano Septemba 17,2025.
Makulilo amesema lengo la kuandaa kongamano hilo ni kuwakutanisha wadau wa sekta mbalimbali zikiwepo binafsi, asasi zisizo za kiserikali ,vyuo vikuu , washirika wa maendeleo na wananchi lengo likiwa ni kujadili kwa kina juu ya fursa za mwenendo wa kiuchumi nchini Tanzania kuelekea Dira 2050.
Amesema awali, Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kuzindua Dira hiyo alitoa maelekezo sita kutaka wananchi,watendaji na wadau wapatiwe elimu ili kuwezesha kushiriki kikamilifu katika kuchangia .
"Miongoni mwa maagizo ushirikishwaji kwenye utekeleza wa mpango kwa kuweka mikakati ya Mawasiliano ya elimu kwa umma na uhamasishaji kuhusu dira ili watendaji na wananchi waelewe nafasi. na mchango wao,"amesema .
Kuhusu kuanza utekelezaji wake.
Makililo amesema Dira hiyo itaanza kutekelezwa katika mwaka wa fedha Julai Mosi 2026 huku mpango wa maandalizi ya bajeti utaanza mwishoni mwa mwaka 2025 ili wananchi , watendaji na wadau waweze kushiriki katika utekelezaji wake kupitia bajeti mpya ili waweze kutoa mapendekezo.
" Tanzania itakuwa na mpango wa maendeleo wa Taifa kwa miaka mitano kuanzia 2025/26 mpaka 2029/30 ambao utajengwa kwa kuzingatia hali halisi ya utekelezaji wake,"amesema.
Profesa ,Makulilo amesema kuwa katika kongamano hilo miongoni mwa mada zitakazo jadiliwa ni pamoja na madhumuni ya dira ya 2050 na misingi ya uchumi jumuishi kuelekea mpango huo na kuangazia mafanikio ya utekelezaji wa maendeleo ya Taifa kwa miaka mitano ambayo inaishia 2020/21mpaka 2025/2026.
Nyingine ni nafasi ubia katika uchumi kama msingi wa maendeleo jumuishi na endelevu nchini Tanzania huku wachokoza mada wakiwa ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ,Dk Fredy Msemwa na Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Ubia cha Sekta Binafsi na Umma,David Kafulila.
Wengine ni Mbunge wa Afrika Mashariki, Gradness Salema ,Mtendaji Mkuu,Jumuiya ya Wafanyabiashara kundi la wanawake, Dk Mwajuma Hamza ,sambamba na Prof, Humphrey Moshi kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam.
Kwa upande wake Mratibu wa Miradi ya Ubia kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara,Msoloni Dakawa amesema wanatarajia ushiriki wa wakuu wa mikoa wa Mbeya na Songwe sambamba na Wakuu wa Wilaya 10.
Wengine ni wakurugenzi 12 kutoka halmashauri kutoka Mbeya na Songwe ,lakini wapo Makatibu Tawala wa viwanda uchumi na uzalishaji,Kamishna msaidizi wa ardhi,wakuu wa idara ya maendeleo ya jamii,wakuu wa idara 228 .
"Pia, itahususisha wanasiasa na wazee wa mila (machifu) ,viongozi wa dini ,vijana na wananchi wa kawaida lengo ni kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan kufikia makundi yote katika kuchangia Dira ya Maendeleo ya Uchimi wa Taifa ifikapo 2050, "amesema.
Kauli za wadau.
Mkazi wa Jijini hapa na kijana Mhitimu wa elimu ya juu ,Alex Mturo amesema ujio wa kongamano hilo lije na suruhisho la changamoto ya fursa za changamoto ya kiuchumi,ajira kwa vijana ifikapo 2050,"amesema.
Mwisho.