Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

75 wakamatwa Tanga katika operesheni maalumu za Polisi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchuguzi akitoa taarifa za matukio kwa waandishi wa habari mkoa wa Tanga.

Muktasari:

  • Jumla ya watu 75 wamekamatwa mkoani Tanga kufuatia operesheni maalumu za Jeshi la Polisi zilizolenga kukomesha uhalifu ikiwemo wizi, dawa za kulevya na uharibifu wa miundombinu.

Tanga. Watu 75 wamekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga kufuatia msako maalumu uliofanyika katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha usalama wa raia na mali zao.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi, amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na operesheni zilizoendeshwa kuanzia Mei hadi Juni 18, 2026.

“Katika kipindi hicho tumekamata watuhumiwa 75 wa makosa mbalimbali kupitia msako unaoendelea mkoani Tanga,” amesema Mchunguzi.

Amesema katika operesheni hizo, watuhumiwa sita walikamatwa kwa kuhusika na uharibifu wa miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa kuiba vifaa vya transfoma katika Kijiji cha Gomba Lamu, Kata ya Makuyuni, Wilaya ya Korogwe.

“Vitendo hivyo vimesababisha hasara na kukatika kwa huduma ya umeme kwa wananchi,” amesema.

Kuhusu wizi wa kuvunja nyumba, Kamanda amesema watuhumiwa 15 walikamatwa ambapo 10 kati yao tayari wamefikishwa mahakamani na kesi zinaendelea.

“Jeshi la Polisi linaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya wizi na uvunjaji wa nyumba,” amesema.

Katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya, amesema watuhumiwa 16 walikamatwa wakiwa na bangi, mirungi na vifaa vingine haramu, ikiwemo kete 122 za bangi, misokoto 57 na bunda 967 za mirungi.

“Operesheni hizi zinaendelea katika wilaya za Pangani, Mkinga na Korogwe,” amesema.

Kuhusu pombe haramu, mtuhumiwa mmoja alikamatwa akiwa na lita 40 za gongo pamoja na vifaa vya kutengenezea pombe hiyo.

“Hatutavumilia uzalishaji wa pombe haramu kwa kuwa ni hatari kwa afya na usalama wa jamii,” amesema.

Katika uhalifu wa kutumia silaha, watuhumiwa 12 walikamatwa, huku pikipiki 20 zisizo na namba za usajili zikikamatwa na nyingine kutambuliwa na wamiliki wake.

Kuhusu simu zilizoibiwa, Polisi walipokea taarifa za simu 30 zilizoibwa ambapo 15 zimepatikana na zinaendelea kutambuliwa.

“Tunawahimiza wananchi kutoa taarifa ili kusaidia kurejesha mali zao,” amesema.

Aidha, amesema watu 25 walikamatwa kwa makosa ya usalama barabarani, ikiwemo kuendesha bila leseni na mwendo kasi.

“Sheria za barabarani lazima zifuatwe ili kuepusha ajali,” amesema.

Kuhusu kesi mahakamani, amesema baadhi ya watuhumiwa wamehukumiwa vifungo mbalimbali, ikiwemo kifungo cha miaka 30 kwa makosa ya dawa za kulevya na ubakaji.

“Haya ni matokeo ya ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na vyombo vya sheria,” amesema.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limewataka wananchi kuendelea kushirikiana kwa kutoa taarifa za uhalifu ili kuimarisha usalama.