Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Abiria 20 wanusurika kifo ajali ya lori, Coaster

Basi lililogongwa na lori la mafuta lililokuwa likitokea Tunduma kwenda Mpemba katika Barabara ya Tunduma Mbeya

Songwe. Zaidi ya abiria 20 waliokuwa wakisafiri kwa basi dogo aina ya Coaster lililotokea Tunduma kwenda Mpemba katika Barabara ya Tunduma Mbeya wamenusurika kifo baada ya lori la mafuta kufeli breki na kuligonga basi hilo.

Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo Dickson Kapungu amesema tukio hilo lilitokea jana jioni muda wa saa 1usiku katika eneo la Sogea (kwa Toronto) ambapo lori lililobeba mafuta kufeli breki na kuligonga kwa mbele basi hilo kisha lori hilo kutumbukia mtaroni.

"Kwa bahati nzuri magari yote mawili yalikuwa katika mwendo mdogo vinginevyo tungeshuhudia mambo mengine," amesema Kapungu.

Amesema abiria wote wakiwemo madereva walinusulika na kutoka salama.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Theopista Mallya alipopigiwa simu Ili aweze kuzungumza suala hilo simu ilipokewa na msaidizi wake ambaye hakujitanbulisha na amesema kamanda huyo yupo kikaoni.