Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ACT Wazalendo: Muaji ya Enock matokeo ya kuporomoka kwa maadili ya viongozi

Muktasari:

  • Jana Alhamisi Julai 3,2025 picha ya mjongeo iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii ikiwaonyesha watuhumiwa hao wakiwa wamemfunga Enock na kumpeleka porini na kuanza kumpiga kwa kutumia fimbo sehemu mbalimbali za mwili.

Rukwa/ Simiyu . Chama ACT Wazalendo, kimesema kutokea kwa matukio kama la kupigwa hadi kuuawa kwa kijana Enock Mhangwa mkoani Geita, ni matokeo ya kuporomoka kwa maadili kwa baadhi ya viongozi sambamba na utawala wa sheria.

Jana Alhamisi Julai 3, 2025 picha ya mjongeo iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii ikiwaonyesha watuhumiwa hao wakiwa wamemfunga Enock na kumpeleka porini na kuanza kumpiga kwa kutumia fimbo sehemu mbalimbali za mwili.

Baada ya picha mjongeo kusambaa leo Julai 4, 2025 Jeshi la Polisi limetangaza kuwakamata watu wawili akiwamo Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Liyobahika, Fredinand Antony kwa tuhuma za mauji ya kijana huyo huku watuhumiwa wengine akiwamo askari mgambo wakisakwa.

Katika picha ya mjongeo hiyo iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii, iliwaonyesha watuhumiwa hao wakiwa wamemfunga kamba mikononi kijana huyo na kumpeleka porini kisha wakaanza kumpiga kwa kutumia fimbo sehemu mbalimbali za mwili.

Hayo yameelezwa leo, Ijumaa Julai 4, 2025 na Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo (Bara), Issihaka Mchinjita alipozungumza na wananchi wilayani Busega mkoani Simiyu.

Ameelaani tukio hilo, huku akidai ni matokeo ya kuporomoka kwa utawala wa sheria.

"Kwa sababu utawala wa sheria unapoporomoka, matendo ya kikatili hutamalaki na watu kuona kuwa matendo ya kawaida," amesema kiongozi huyo.

Amesema ingawa tukio hilo limetokea kitambo, jana ndiyo Jeshi la Polisi linapata taarifa na kutangaza kuchukua hatua.

Mchinjita amedai hatua hiyo ni kiashiria kuwa Serikali imeshindwa kuwasimamia raia wake.

Kwa upande wake Kiongozi mstaafu wa chama hicho, Zitto Kabwe amehoji kwa nini tukio limetokea kitambo lakini taarifa zimechelewa kutolewa

Katika maelezo yake Zitto, "tukio limetokea Juni 26 mwaka huu, leo Julai 4, tangu kutokea tukio la kijana yule Jeshi la Polisi limetoa taarifa leo. Ina maana ile video ya kijana isingeonekana, polisi wasingetoa taarifa? Au lisingetimiza wajibu wake wa kukomesha uhalifu?," amehoji na kuongeza;

"Jeshi la polisi limetoa kauli rasmi leo, baada ya video kuonyesha watendaji wakimtenda Enock. Kwa nini polisi wamekuwa kimya, si bahati mbaya...," amedai Zitto.

Amesema haiingii akilini mtendaji kumpiga mwananchi hadi anakufa halafu inachukua muda mrefu taarifa zake zinachukua muda mrefu kujulikana kwa umma.

“Si kwa sababu ya uchunguzi wao bali kwa sababu kuna watu wameweka kwenye mtandao," amesema Zitto.


Hatususi uchaguzi

"Historia inaonyesha ukiwaachia au kususia watawala huwa hawana tabia ya kurudi nyuma, bali wanasonga mbele, Uganda wapinzani wanalalamika kuibiwa lakini hata siku moja umsikii Bob Wine anasema wanasusia uchaguzi."

“Kama watu wamechoka mapambano wasiwachoshe wananchi, mapambano yanaendelea.Kuna watu watapambana lakini hawatakula matunda ya mapambano hayo, twendeni tukapambane naamini tutafanikiwa tususie uchaguzi," amesema Zitto.

Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake ya ACT Wazalendo, Janeth Rithe amesema, "tupo kwenye ziara kwa ajili ya kuzungumza na Watanzania wajue Taifa lilipotoka na linakoelekea kupitia operesheni ya majimaji.

"Lazima Watanzania tukubali mabadiliko ili Tanzania isonge mbele, hatuwezi kuondokana na changamoto hizi kama hatutaiondoa CCM madarakani," amesema Rithe.

Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo (Bara), Ester Thomas amesema chama hicho kinaamini katika vijana ndio kinawapata fursa za uongozi ili kutetea masilahi ya Watanzania.

“Watu Rukwa mkiwemo vijana kazeni buti chagueni shirikini uchaguzi ili viongozi mnawahitaji ili kuwaletea maendeleo," amesema Thomas.

Waziri Kivuli wa Nishati na Katibu wa Idara ya Haki za Binadamu wa ACT Wazalendo, Mbarala Maharagande amesema licha ya CCM bado hawajatatua changamoto za kijamii ikiwemo sekta za afya, elimu na miundombinu.

" ACT Wazalendo tunasema hatutachoka kukikosoa Chama cha Mapinduzi, hatutawaogopa kamwe. Hatuna sababu ya kurudi nyuma katika mapambano ya kuiondoa CCM," amesema Maharagande.

Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mkoa wa Kigoma, Kiza Mayeye amesema chama hicho hakisusii uchaguzi kwa sababu anayesusiwa si muungwana hivyo hawatakuwa tayari kukisusia chama tawala cha CCM.