Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ada ya maegesho ya magari Kilimanjaro kulipwa kwa mtandao

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai

Muktasari:

  • Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amesema kuanzia Aprili Mosi 2022 ada za maegesho ya magari katika barabara zinazomilikiwa na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura), zitakuwa zikilipwa kwa njia ya mtandao badala ya fedha taslimu.

  

Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amesema kuanzia Aprili Mosi 2022 ada za maegesho ya magari katika barabara zinazomilikiwa na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura), zitakuwa zikilipwa kwa njia ya mtandao badala ya fedha taslimu.

Kagaigai amesema hayo jana Machi 24, 2022 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu kuanza kutumia mfumo huo.

Kagaigai amesema Serikali imeamua kuja na mfumo huo kuondoa changamoto mbalimbali zilizokuwa zikijitokeza katika ukusanyaji wa ada za maegesho ya magari kwa njia ya kulipia fedha taslimu

Amesema lengo ni kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali yatakayosaidia maboresho na miundombinu ya barabara, kutoa fursa kwa mteja kulipa ushuru wa maegesho kwa saa, siku, wiki au mwezi.

 “Kuanzia Aprili Mosi mwaka huu, malipo yote ya mkoa wa Kilimanjaro yatafanyika kwa kutumia kumbukumbu namba ya malipo na hivyo hakutakuwa na utoaji wa pesa tasilimu kama ilivyo sasa.

 “Huku nyuma kulikuwa na uvujaji wa mapato ya Serikali lakini mfumo huu utasaidia na kuimarisha ukusanyaji wa mapato” amesema.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (Tarura) mkoani humo, Nicholous Francis amesema wamejipanga kutoa elimu kwa wananchi wote ili kupunguza malalamiko