Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Adaiwa kutumia jina la William Lukuvi kujipatia Sh2.1 milioni

Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mtu mmoja aliyejifanya kutumia jina la aliyekuwa Waziri wa ardhi,William Lukuvi na kwamba amemtuma na kuendesha mafunzo ya ujasiriamali visivyo halali Mkoani Kilimanjaro katika ukumbi wa polisi Moshi  na kujipatia Sh2.1milioni kwa wanafunzi wajasiriamali kama gharama za cheti. Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

  • Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mtu mmoja (jina limehifadhiwa) akidaiwa kutumia jina la Waziri wa zamani, William Lukuvi kujipatika Sh2.1 milioni kwa kuendesha mafunzo ya ujasiriamali katika ukumbi wa Polisi Moshi mjini.

Moshi. Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mtu mmoja ambaye ni mkazi wa Mabibo Jijini Dar es salaam (jina linahifadhiwa) akitumia jina la Waziri wa zamani, William Lukuvi kuendesha mafunzo ya ujasiriamali mkoani Kilimanjaro na kujipatia Sh2.1 milioni kupitia mafunzo hayo.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Simon Maigwa amethibitisha kukamatwa kwa mtu huyo, akisema alikuwa akijipatia Sh35,000 kwa kila mshiriki wa mafunzo hayo huku akiwaahidi kuwalipia kila mmoja Sh300,000 kama ada baada ya kuhitimu mafunzo hayo na kwamba atawapatia ajira.

Kamanda Maigwa amesema baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema wakati akiendesha mafunzo hayo katika ukumbi wa polisi Moshi, Jeshi la Polisi lilitumia mbinu za kumnasa mtu huyo.

"Baada ya kupata taarifa hizi jeshi la polisi tuliwasiliana na viongozi ambao mtuhumiwa huyu alikuwa akiwataja ambapo walimkana na kwamba hawamjui, hivyo tunaendelea kumshikilia kwa hatua zaidi," amesema Kamanda Maigwa.

Mtuhumiwa huyo amekuwa akiendesha mafunzo hayo ya ujasiriamali katika mikoa mbalimbali ya Dar es salaam, Tanga, Morogoro, Arusha, Mbeya na Tanga kwa kujipatia kipato isivyo halali.