Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Afariki dunia kwa kutumbukia kwenye kisima cha mafuta

Baadhi ya askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Kilimanjaro wakiwa wamebeba mwili wa kijana Shalom Tarimo (21) aliyefariki baada ya kutumbukia kwenye kisima cha mafuta eneo la Moshi mkoani Kilimanjaro leo Agosti 9, 2024. Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

  • Mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Shalom Albert Tarimo(21), mkazi wa  Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye kisima kilichokuwa kikitumika kuhifadhia mafuta ya dizeli.

Moshi. Mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Shalom Albert Tarimo (21), mkazi wa msaranga, Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye kisima kilichokuwa kikitumika kuhifadhia mafuta ya dizeli  katika kituo  kimoja cha mafuta kilichopo katikati ya mji wa Moshi.

Kituo hicho cha mafuta kinachodaiwa kumilikiwa na mfanyabiashara maarufu mjini hapa, kilikuwa kikifanyiwa ukarabati  baada ya kukaa kwa muda mrefu.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, Mrakibu Msaidizi wa Jeshi hilo, Jeremiah Mkomagi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho leo Agosti 9, 2024 ambapo amesema kijana huyo kabla ya kupatwa na mauti alikuwa akifanya kazi ya kusafisha kisima hicho.

"Majira ya saa 5:23 asubuhi tulipokea taarifa ya kuwepo kwa tukio la mtu kutumbukia kwenye kisima cha mafuta ambacho kilikuwa kikifanyiwa marekebisho kukipima kama kinaendelea kufaa kufanya kazi. Baada ya kupata taarifa hizi tulifika mara moja na kuanza shughuli za uokoaji kutoa mwili wa marehemu kwenye kisima,"

Kamanda Mkomagi, amesema kisima hicho kilikuwa kikitumika kuhifadhia mafuta ya dizeli lita 40,000 na kwamba wakati tukio hilo linatokea kulikuwepo na dizeli iliyobaki ndani ya kisima hicho wakati walipokuwa wakifanya usafi.

"Maji yalikuwa yamechanganyikana na dizeli ambayo ilikuwa imebaki ndani ya kisima wakati walipokuwa wakifanya usafi, hivyo askari wetu waliingia ndani ya kisima kwa kutumia vifaa maalum kwa kuchukua tahadhari dhidi ya afya zao na hivyo tuliweza kuupoa mwili wa marehemu ambao umepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi," amesema Kamanda Mkomagi

Mmoja wa askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Kilimanjaro wakati akiopoa mwili wa kijana, Shalom Tarimo (21) mkazi wa msaranga aliyedumbukia kwenye kisima cha kuhifadhia mafuta Moshi mkoani Kilimanjaro leo Agosti 9, 2024.

Aidha, Mkomagi ametoa rai kwa wamiliki wa vituo vya mafuta kuhakikisha wanapofanya usafi kwenye visima vya mafuta, wachukue tahadhari ili kuepusha majanga yanayoweza kujitokeza ikiwemo watu kupoteza maisha.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Msami Mndeme amesema wakati tukio hilo linatokea,  alikuwa anapita pembezoni mwa kituo hicho cha mafuta na kusikia wito  na alipokimbilia eneo la tukio alishuhudia kijana huyo akiwa ndani ya kisima hicho huku jitihada za kumwokoa zikiendelea licha ya kwamba hazikufanikiwa.

"Nilikuwa napita njia niliona Mzee mmoja ameweka mkono kichwani anapiga kelele nilipofika karibu kumbe kuna kijana aliyetumbukia ndani ya kisima watu walikuwa wanahaha kumwokoa lakini ikashindikana," amesema shuhuda huyo.

Hata hivyo jitihada za kumpata mwendeshaji wa kituo hicho cha mafuta hazikuzaa matunda na hata mmoja wasimamizi wa kituo hicho aliyekuwepo kwenye eneo hilo,  hakutaka kutoa ushirikiano  kwa waandishi wa habari na badala yake   akawataka waandishi kuondoka eneo hilo.