Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Afariki kwa kuchomwa mkuki katika fumanizi Singida

Mkulima achomwa mkuki mgongoni

Muktasari:

  • Mkazi wa kijiji cha Merya Tarafa ya Ilongero mkoani Singida, Innocent Dule (49), amefariki dunia baada ya kudaiwa kuchomwa mkuki mgogoni, wakati akifanya mapenzi na mke wa mtu.

Singida. Mkazi wa kijiji cha Merya Tarafa ya Ilongero mkoani Singida, Innocent Dule (49), amefariki dunia baada ya kudaiwa kuchomwa mkuki mgogoni, wakati akifanya mapenzi na mke wa mtu.

Dule anadaiwa kuchomwa mkuki huko mgongoni na Simon Mwangi (58), baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mke wa Mwangi shambani, ingawa muda wa fumanizi hilo haukutajwa.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, ACP Stella Mutabihirwa, amesema tukio hilo ni limetokea Julai 9, 2023 na mtuhumiwa bado anatafutwa na Polisi.

Kamanda Mutabihirwa amesema japo mtuhumiwa anadaiwa kukimbia kukwepa mkono wa sheria, Jeshi la Polisi wanaendelea kumsaka ili aweze kufikishwa mahakamani na hivyo sheria ichukue mkondo wake.

Taarifa za uhakika kutoka eneo la tukio, zinadai kuwa mtuhumiwa Mwangi, alipewa taarifa na marafiki zake kuwa mke wake anafanya mapenzi shambani akiwa na Dule (Marehemu), na kwamba ilikua ni kawaida yao kabla ya kuwekewa mtego huo.

(Imeandikwa na Gasper Andrew)