Afikishwa mahakamani akidaiwa kukutwa na viungo vya binadamu

Mshtakiwa Salum Nkonja( wa kwanza kushoto) akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kusomewa kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya kukutwa na viungo vya binadamu. Picha na Hadija Jumanne

Muktasari:

  •  Mkazi wa Maswa, mkoani Simiyu, Salum Nkonja maarufu kama Emmanuel Nkonja, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka 11 yakiwemo ya kukutwa na chuchu za binadamu, sehemu za siri tano za wanawake na mafuvu mawili ya kichwa cha binadamu.


Dar es Salaam. Mkazi wa Maswa, mkoani Simiyu, Salum Nkonja maarufu kama Emmanuel Nkonja, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka 11 yakiwemo kukutwa na chuchu za binadamu, sehemu za siri tano za wanawake na mafuvu mawili ya kichwa cha binadamu.

Nkonja amefikishwa mahakamani hapo leo, Juni 21, 2022 na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi namba 32/2022 na wakili wa Serikali, Caroline Materu, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhani Rugemalira.

Mshtakiwa anadaiwa kutenda makosa yake, Kati ya Oktoba 30, 2017 na Novemba 30, 2017 katika eneo la Ubungo lililopo Manispaa ya Ubungo.