Ajali yaua konda, abiria

Muktasari:
- Konda wakampuni ya Superfeo Express Gasto Mapunda (28) amefariki dunia na abiria mwingine Rehema Kafwimbi (39) amevunjika mguu wa kulia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupata ajali.
Songea. Konda wakampuni ya Superfeo Express Gasto Mapunda (28) amefariki dunia na Rehema Kafwimbi (39) amevunjika mguu wa kulia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutokaMbinga kwenda Mbeya kugonga Roli la makaa ya Mawe kwa nyuma.
Akizungumza na Mwananchi Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, ACP Joseph Konyo alisema,ajali hiyo imetokea majira ya saa moja na robo asubuhi katika eneo la Kijiji cha Sinai Kata ya Lilambo tarafa ya Songea Magharibi Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma ikihusisha basi lenye namba za usajili T.843DQV YUTONG ya kampuni ya superfeo express
Likitokea Mbinga kwenda Mbeya, basi hilo lililokuwa likiendeshwa na Ayoub Matomondo (35) mkazi wa Mfaranyaki Songea liligonga gari lenye namba za usajili KDU 142G/ZD 5792 aina ya TATA-NOPAS kampuni ya ROY HAULIERS LTD -KENYA lililokuwa nashehena ya makaa ya mawe ambayo yalikuwayakipelekwa Kenya na likiendeshwa na Paul Nzou (47).
Alisema,Konda wa basi hilo amefariki papo hapo na Rehema Kafwimbi mtakwimu wa Benjamin Mkapa Foundation ambaye alikuwa abiria wa basi hilo amevunjika mguu wa kulia na amelazwa hospitali ya misheni peramiho kwa matibabu
Kamanda Konyo amesema, chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi kujaribu kupita gari la mbele yake lori bila kuchukua tahadhari ya kutosha hivyo kuligonga kwa nyuma.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya misheni peramiho kusubiri uchunguzi wa daktari dereva wa basi hilo amekamatwa kwa hatua za kisheria.
“Natoa wito kwa madereva na watumiaji wote wa vyanzo vya moto wa Mkoa wa Ruvuma kuwamakini kwa kuhakikisha wanachukua tahadhari na kufata sheria za usalama barabarani ili waweze kuepukana na ajali zisizo na lazima kwao na kwa watumiaji wengine wa barabara,”alisema