Alichozungumza Sabaya baada ya Hukumu

Muktasari:

  •  Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amewataka ndugu zake wasiogope kwani Mungu yupo kazini.

  

Arusha. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amewataka ndugu zake wasiogope kwani Mungu yupo kazini.

Amezungumza hayo leo Ijumaa Oktoba 15, 2021 muda mfupi baada ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Arusha, Odira Amworo kutoa hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela baada ya kumtia hatiani kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.

“Ndugu zangu msiogope Mungu yupo kazini” amesema Sabaya.

Agosti 24 mwaka huu, Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura walikamilisha kujitetea mahakamani hapo baada ya Jamhuri kukamilisha mashahidi 11 na vielelezo vinane.

Sabaya alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Juni 4, mwaka huu baada ya kukamatwa Mei 27 wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.