Wengi wajitokeza kusikiliza hukumu kesi ya Sabaya na wenzake

Friday October 01 2021
kesi sabayapicc
By Mussa Juma

Arusha. Idadi kubwa ya watu imejitokeza leo Ijumaa Oktoba Mosi, 2021 katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kusikiliza hukumu ya kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya na wenzake wawili.

Watu wameanza kufika mahakamani hapo saa moja asubuhi wakiwemo maafisa wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, ndugu, na baadhi ya mawakili waliokuwa wakifuatilia mwenendo wa kesi hiyo.

"Nimewahi kusikiliza hukumu nataka kuona haki ikitendeka" amesema Peter John Kimaro ambaye mmoja wa watu wanaofuatilia kesi hiyo.

Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa leo na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Odira Amworo baada ya kusikiliza kesi dhidi ya Sabaya na wenzake wawili kwa miezi miwili na nusu iliyopita.

Hadi kufikia saa 3:30 Sabaya bado alikuwa hajafikishwa mahakamani hapo.


Advertisement


Advertisement