Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyekutwa na majongoo bahari augua, kesi yashindwa kuendelea

Muktasari:

  • Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi inayomkabili raia wa China, Wei Zhang (54) anayedaiwa kukutwa na majongoo hadi Julai 18, 2023 kutokana na leo Jumatatu, Mahakama hiyo kuelezwa mshatkiwa ni mgonjwa.

Dar es Salaam. Kesi ya kukutwa na kilo 4.10 za majongoo bahari ambayo yapo hatarini kutoweka, inayomkabil raia wa China, Wei Zhang (54) imeshindwa kuendelea baada ya mshtakiwa huyo kuugua.

 Zhang ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam ameshindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu, baada ya kuugua.

Mdhamini wa shtakiwa huyo, Ismail Mbajo ameieleza Mahakama hiyo, leo Jumatatu Julai 10, 2023 wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya Zhang kusomewa maelezo yake na kisha hukumu.

Zhang alitakiwa kusomewa hukumu yake baada ya kukiri shtaka lake wiki iliyopita.

Mbajo amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo kuwa, Zhang ni mgonjwa na leo ameshindwa kufika mahakamani hapo kusikiliza kesi yake.

Mdhamini huyo baada ya kueleza hayo, wakili wa Serikali, Tumaini Maingu akishirikiana na Cathberth Mbilingi, alidai kutokana na mshtakiwa kuwa mgonjwa wanaomba tarehe nyingine ili waje kumsomea maelezo yake.

"Kesi imeitwa leo kwa ajili ya kumsomea maelezo yake, lakini tumepata taarifa kutoka kwa mdhamini wake kuwa Zhang ni mgonjwa na leo ameshindwa kufika mahakamani hapa," amedai Wakili Maingu.

Hakimu Shaidi baada ya kusikiliza maelezo ya upande wa mashtaka, ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 18, 2023 kwa ajili ya kusomewa maelezo yake.

Julai 6, 2023 mshtakiwa alikiri kukutwa na majongoo hayo baada ya kukumbushwa shtaka lake wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kusomewa hoja za awali (HP).

Baada ya kukiri shtaka hilo, Serikali iliomba ahirisho fupi ili ilete vielelezo mahakamani hapo, ambavyo ni kilo nne za majongoo bahari.

Katika kesi ya msingi, mshtakiwa anakabiliwa kesi ya jina namba 113/2023.

Anadaiwa kutenda kosa hilo April 7, 2023 katika mtaa wa Kumbukumbu uliopo Kinondoni.

Siku hiyo ya tukio, mshtakiwa huku akijua jamii hiyo ya majongoo bahari ipo hatarini kutoweka, alikutwa akiwa na kilo 4.10 za majongoo bahari( Sea Cucumber) kinyume cha sheria.

Kwa mara ya kwanza, mshtakiwa alifikishwa mahakamani hapo Juni 26, 2023 na kusomewa kesi hiyo.