Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Android 17 imeachiwa rasmi angalia hapa maajabu yake, ‘full AI’


Muktasari:

  • Mfumo huo wa uendeshaji wa Google umeanza na simu za Google Pixel kwanza.



Dar es Salaam. Kampuni ya teknolojia ya Google imeachia rasmi toleo jipya la mfumo wake wa uendeshaji wa simu, Android 17, likija na maboresho makubwa katika matumizi ya akili unde (AI), usalama wa taarifa, pamoja na uwezo wa kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja.

Toleo hilo limeanza kupatikana kwenye simu za Google Pixel kuanzia Pixel 6 na kuendelea, huku watengenezaji wengine wa simu za Android kama Samsung, Xiaomi, Oppo na Honor wakitarajiwa kuanza kusambaza masasisho (updates) hayo kwa watumiaji wao baadaye mwaka huu.

Android ni mfumo wa uendeshaji wa simu za mkononi uliotengenezwa na Google kwa kushirikiana na jumuiya ya watengenezaji wa programu kupitia Android Open Source Project (AOSP).

Mfumo huo hutumika kuendesha vifaa mbalimbali vikiwemo simu janja, kompyuta vishkwambi, televisheni janja, saa za mkononi na vifaa vingine vinavyotumia intaneti.

Kwa lugha rahisi, Android ni programu kuu inayoratibu mawasiliano kati ya vifaa vya ndani vya simu kama kamera, betri, prosesa na programu mbalimbali zinazotumiwa na mtumiaji.

Mfumo huo hufanya kazi kwa kusimamia matumizi ya kumbukumbu, kuendesha programu, kulinda taarifa za watumiaji na kuhakikisha mawasiliano kati ya vifaa na huduma za mtandaoni yanafanyika kwa ufanisi.

Takwimu za kampuni ya utafiti wa masoko ya teknolojia zinaonyesha Android ndiyo mfumo wa uendeshaji unaotumika zaidi duniani, ukibeba sehemu kubwa ya soko la simu janja.

Umaarufu wake unatokana na uwezo wa kufanya kazi kwenye simu za bei tofauti pamoja na uhuru unaowapa watengenezaji kuboresha mwonekano na huduma kulingana na mahitaji yao.

Miongoni mwa sifa kuu za Android ni uwezo wa kubinafsisha mwonekano wa simu, kupakua programu kupitia Google Play Store, kuunganisha huduma za Google kama Gmail, Ramani na Hifadhi ya Google, pamoja na kuruhusu watengenezaji kutengeneza programu kwa urahisi.

Katika Android 17, Google imeweka mkazo mkubwa kwenye matumizi ya AI, usalama na uzalishaji.


Nini kipya kwenye android 17

Moja ya maboresho makubwa ni huduma ya Bubbles, inayoruhusu mtumiaji kufungua programu kwa juu ya skrini ili kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja bila kufunga programu nyingine.

Pia, Android 17 imeongeza kipengele cha Screen Reactions, kinachowezesha mtumiaji kurekodi kinachoendelea kwenye skrini huku akijirekodi kwa kamera ya mbele kwa wakati mmoja, jambo linalotarajiwa kuwasaidia watengeneza maudhui na wakufunzi wa mtandaoni.

Kwa upande wa usalama, mfumo huo umeboreshwa kwa kuongeza ulinzi dhidi ya wizi wa simu, udhibiti wa ruhusa za programu kupata taarifa za eneo la mtumiaji na uwezo wa kushiriki mawasiliano machache badala ya orodha nzima ya namba za simu.

Aidha, Android 17 imeboresha matumizi ya betri, usimamizi wa kumbukumbu na utendaji wa programu ili kuongeza kasi ya simu hata kwa vifaa vya zamani. Maboresho hayo yanatarajiwa kusaidia watumiaji kupata uzoefu bora zaidi wanapotumia programu nyingi kwa wakati mmoja.


Utofauti wake na Android 16

Android 17 si mabadiliko makubwa ya mwonekano kama ilivyokuwa kutoka Android 12 kwenda 13, lakini imejikita zaidi katika uboreshaji wa matumizi ya AI, kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja (multitasking) na usalama.

Uwezo wa AI, katika Android 16, Gemini ilikuwa inapatikana ndani ya programu maalumu, lakini hivi sasa imeunganishwa zaidi kwenye mfumo kupitia Gemini Intelligence.

Katika utendaji kazi Android 16, ilikuwa na uwezo wa kurekodi skrini pekee lakini sasa hivi inaweza kurekodi skrini na uso wako kwa kamera ya mbele kwa wakati mmoja

Katika usalama vipengele vya msingi vya kupambana na wizi kwa sasa ulinzi umeimarishwa zaidi dhidi ya wizi wa simu na matumizi yasiyoidhinishwa.


Jinsi ya kuingiza Androdi 17

1. Fungua Mipangilio (Settings).

2. Chagua Mfumo (System) au About phone kulingana na aina ya simu yako.

3. Bonyeza Software update, System update au Check for updates.

4. Ikiwa Android 17 inapatikana, utaona ujumbe wa Download and install.

5. Unganisha simu kwenye Wi-Fi na uhakikishe betri ina zaidi ya asilimia 50 kabla ya kuanza kusasisha.


Kwa simu za Samsung, Xiaomi, Oppo, OnePlus, Vivo na watengenezaji wengine, utapata Android 17 baada ya kampuni husika kuandaa toleo lake maalumu la mfumo huo, kama vile One UI, HyperOS au ColorOS. Hii inaweza kuchukua wiki au miezi kadhaa baada ya uzinduzi rasmi wa Android 17.