Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anna Mghwira kuzikwa Jumatatu Arusha

Muktasari:

Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake jijini Arusha Jumatatu Julai 26 mwaka huu.

Moshi. Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake jijini Arusha Jumatatu Julai 26 mwaka huu.

Mghwira alifariki dunia jana Julai 22 katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru jijini Arusha alikokuwa akipatiwa matibabu.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Julai 23, 2021 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amesema mkoa huo umebeba jukumu la kuandaa mazishi ya Mghwira.

"Taarifa za awali ni kwamba tutampumzisha mama Anna Mghwira kwenye makazi yake ya milele Julai 26 mwaka huu jijini Arusha siku ya Jumatatu, taratibu za mazishi kwa sasa zinaendelea,"amesema Kagaigai.

Mghwira ambaye alikuwa mgombea wa Urais katika Uchaguzi Mkuu 2015 aliteuliwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli kuwa mkuu wa Mkoa huo mwaka 2017 akitokea chama cha ACT Wazalendo.