Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Asasi za kiraia zataka maboresho ya mifumo, sera

Msimamizi wa Miradi Foundaton For Civil Society (FCS), Nicolaus Lekule akiwaeleza waandishi wa habari sababu za taasisi yake kufafadhili miradi mbalimbali ya kijamii.

Dar es Salaam. Serikali imetakiwa kurekebisha mifumo, sera na taratibu za kusimamia na kupokea taarifa kutoka Asasi za kiraia badala ya taasisi nyingi kushughulikia jambo linalofanywa na nyingine. 

Asasi za kiraia zimependekeza iwepo taasisi moja ya Serikali ambayo watalazimika kuripoti kwa zaidi ya taasisi moja zilizo chini ya Serikali jambo linalowapa usumbufu.

Pendekezo hilo wamelitoa jana, Jumatatu Desemba 18, 2023 walipokuwa kwenye mkutano wa kutathmini shughuli za utekelezaji wa mradi wa Uraia Wetu unaofadhiliwa na Foundaton For Civil Society (FCS) kwa asasi hizo.

Mratibu wa mradi huo wa Uraia Wetu, Kanda ya Kusini, Deogratius Makoti amesema katika mazingira ya sasa ya sayansi na teknolojia kuna haja ya kuwa na mfumo mmoja wa taarifa (one stop centre) utakaokuwa na taarifa zote asasi hizo badala ya ule wa sasa wa kutakiwa kuripoti kwenye kila taasisi inayozihusu.

Amesema wanalazimika kutumia muda mwingi na fedha kwenda huku na kule kukamilisha nyaraka zinazotakiwa na taasisi husika ya Serikali.

“Leo hii wenzetu wanaweza kufanya kazi zao katika eneo moja, kwanini sisi tusifanye hivyo wakati taasisi hizi zote ni za Serikali,” amehoji na kuongeza:

“Kwa mfano unakuta kuna maelekezo kutoka kwa Halmashauri, kwamba kila asasi iripoti kwa Msajili Msaidizi au Ofisa maendeleo na kila mmoja anaweza kutoa ‘fomart’ yake kwa vile anavyoona. Haiishii hapo, hapohapo unaweza kupigiwa simu na Mratibu wa mkoa na yeye anataka umpatie taarifa wakati tayari ulishampatia mtu wa Halmashauri,”amesema Makoti.

“Na ndio pale unasikia Ngo’s nyingi zinalalamikiwa kwamba ni wababaishaji hawatoi taarifa kumbe mifumo yao ndiyo haisomani. Kwa hiyo kwa sababu ya mkanganyiko huo, unachangia nyingine zisiripoti kabisa kwa sababu ya usumbufu au hata kama zimepeleka ripoti zao, unakuta taasisi nyingine haijazipata na mwisho wa siku zinajikuta katika hatari.”

Msimamizi wa Miradi kutoka FCS, Nicolaus Lekule, amesema kuna haja ya kufanyiwa maboresho ya sera zinazosimamia asasi hizo ili kuziwezesha kuendesha shughuli zao kwa ufanisi.

“Tunataka asasi ziwe na mazingira ambayo ni wezeshi kufanya shughuli zake. Tunatarajia kuona mabadiliko ya kisera na kisheria na utekelezaji wake ili asasi hizi zifanye kazi kwa ufanisi zaidi na tunatamani Serikali ielewe ajenda yetu na ifanyie kazi changamoto zozote zinazoonekana kwa sasa.

Lekule amesema katika kufanikisha utekelezaji wa mradi huo wa Uraia Wetu ulioanza Juni 2023, wametoa ruzuku kwa asasi 15 zinazofanya kazi na vijana, wanawake na watu wenye ulemavu na mradi huo unatarajiwa kutekelezwa kwa miaka mitatu.