Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Askari mbaroni akituhumia kwa mauaji

Muktasari:

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia askari wa wanyamapori kwa tuhuma za mauaji ya mtoto Ngatipa Parmao (17) kwa madai ya kuswaga mifugo ndani ya Hifadhi ya Mkomazi.

Mwanga. Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia askari wa wanyamapori kwa tuhuma za mauaji ya mtoto Ngatipa Parmao (17) kwa madai ya kuswaga mifugo ndani ya Hifadhi ya Mkomazi.

Mtoto huyo ambaye ni wa jamii ya kimasai na mkazi wa kijiji cha Pangaroo, wilayani Mwanga anadaiwa kupigwa risasi Julai 6, 2022 na askari ambapo amefariki leo Katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) alikokuwa anapatiwa matibabu.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya hiyo, Abdalah Mwaipaya amekiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba taarifa za kifo cha mtoto huyo wamezipokea leo asubuhi.

"Ni kweli tumepokea taarifa za kifo cha mtoto huyo lakini zaidi tunafuatilia kujua mazingira ya kifo chake   lakini taarifa zilizopo ni kwamba waliingiza mifugo kwenye hifadhi ambapo askari walimkamata ndipo alipoita wenzake wakaja na sime ikabidi askari afyatue risasi angani," amesema Mwaipaya

Amesema wanamshikilia askari huyo kwa mahojiano zaidi.