Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Askari polisi 156 wafukuzwa mafunzo

Muktasari:

  •  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema takribani askari Polisi wanafunzi 156 wamefukuzwa mafunzo ya kijeshi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo za utovu wa nidhamu na kufanya mambo ambayo hayakubaliki ndani ya shule ya Polisi.


Siha, Kilimanjaro. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema takribani askari Polisi wanafunzi 156 wamefukuzwa mafunzo ya kijeshi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo za utovu wa nidhamu na kufanya mambo ambayo hayakubaliki ndani ya shule ya Polisi.

IGP Sirro amesema hayo wakati alipofanya ziara kwenye uwanja wa medani za kivita wilaya ya Siha, West Kilimanjaro katika Shule ya Polisi Tanzania, ambapo pia amewaelekeza wanafunzi hao wa kozi ya awali ya askari Polisi kufuata sheria, kanuni na taratibu za shule hiyo ikiwa pamoja na kudumisha nidhamu ndani ya Jeshi la Polisi.