Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Askari washauriwa kushiriki mazoezi

Baadhi ya askari wa Tanzania bara na Visiwani wakiwa kwenye gwaride la ufunguzi wa Mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMATA) katika uwanja wa Nangwanda Mtwara ambapo michezo mbalimbali itachezwa.  Florence Sanawa

Muktasari:

  • Askari nchini washauriwa kuacha tabia bwete na kushiriki katika mazoezi mbalimbali ya viungo ili kujiepusha na magonjwa yasiyoambukiza.

Mtwara. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Tabia Maulid Mwita amesema kuwa tabia bwete zimekuwa kichocheo cha maradhi hivyo kuwataka askari kuongeza hamasa ya kuchezea michezo mbalimbali.

Kauli hiyo ameitoa leo Alhamisi Februari 9, 2023 wakati akifungua mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (Bamata) katika Uwanja wa Nangwanda ambapo alisema kuwa yapo magonjwa yanasababishwa na mfumo wa maisha tulionao.

“Michezo ni afya kwa binadamu ambapo inajenga afya ya akili mwili na magonjwa mengi ya yasiyoambukizwa husabishwa na mfumo wa maisha tunayoishi unaoambatana na kula vyakula yenye mafuta mengi makopo na kutoshughulisha mwili yaani kutokufanya mazoezi,” amesema.

“Mfano ugonjwa wa kiharusi, figo na maradhi mengine yaliyokithiri katika jamii yetu ambayo husababisha na kutofanya mazoezi na kuleta athari za kiuchumi kwakununua madawa ya kutibia magonjwa hayo,” amesema.  

"Fanyeni mazoezi acheni tabia bwete, michezo huleta amani upendo na furaha mshikamano na kujenga nidhamu pia michezo ni ajira ni chachu ya mafaniko ya mtu, taasisi na taifa kwa ujumla,” amesema.

“Vijana wenye vipaji vya michezo hupewa kipaumbele kwenye nafasi ya ajira ndani ya majeshi yetu nafahamu kuwa marakadhaa michezo imekuwa ikitumika kama mbinu ya kupambana na uharifu,” amesema Mwita.

Mwenyekiti wa Bamata, Brigedia Generali Suleiman Gwaya alisema kuwa tunafanya mashindano ili kuleta hamasa kwa jamii na kuijulisha jamii kuwa michezo ni ajira.

“Michezo ni ajira na pia michezo ni sehemu ya maisha tunahakisha kuwa inafanyika mikoa mbalimbali mwaka jana tulifanya Dodoma mwaka huu Mtwara, mwakani tutachagua wapi tufanye jamii inapaswa itambue kuwa hii michezo ni kama michezo mingine tunawaomba wanamtwara wafike ili waweze kuja kutazama ili wajue nini kinafanyika” amesema.

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa ambaye pia ni Mwenyekiti Kanda Jeshi la Kujenga Taifa, Brigedia Generali Hassan Mabena michezo hiyo inawakutanisha askari wa majeshi yote na kurahisisha ulinzi na usalama wanchi yetu.

“Jeshi la Kujenga Taifa ndio lilishinda mshindi wa jumla mashindano yaliyopita katika michezo ya  mpira wa miguu, pete, basket wanawanake na wanaume, riadha, ngumi, shabaha na judo tumekuja kushindana na kukuza vipaji vinavyochipukia ili kupata timu itakayoenda kushiriki michezo kimataifa,” alisema Brigedia Generali  Suleiman Mbena.