Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Askofu aomba kibali kuombea mvua nchini

Muktasari:

  • Askofu wa kanisa la Good News for All Ministry, Gadi Charles amesema kanisa lake liko tayari kuombea mvua nchini, lakini endapo tu litapata kibali cha viongozi wa hata kipindi hiki ambacho maeneo mengi nchini yameathiriwa na ukame, wao wanaweza kuomba na mvua ikanyesha hata kulijaza bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPPP).

Dar es Salaam. Askofu wa kanisa la Good News for All Ministry, Gadi Charles amesema kanisa lake liko tayari kuombea mvua nchini, lakini endapo tu litapata kibali cha viongozi wa kitaifa.

Amesema hayo leo Januari 4, 2022 katika mkutano wa viongozi wa dini na wanahabari na kubainisha kwamba kama wataruhusiwa kufanya hilo haitakuwa mara ya kwanza kuombea nchi ipate mvua.

“Tumewahi kufanya hivyo na kuombea bwawa la Mtera, Kidatu na kuombea barafu ya Mlima Kilimanjaro,” amesema Askofu Charles.

Amesema hata kipindi hiki ambacho maeneo mengi nchini yameathiriwa na ukame, wao wanaweza kuomba na mvua ikanyesha hata kulijaza bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPPP).

“Kuna watu wanauliza, ukiomba isipotokea? Hiyo sio imani, kwa Mungu hakuna kinachoshindika,” amesema askofu huyo.

Askofu Charles, pia, leo amefanya maombi maalumu ambayo alidai ni ya kubadilisha hali ya hewa ya nchini Marekani.

“Mpango wa Mungu sio mvua ilete maafa, tunaona wenzetu kule Marekani kesho wanatarajia mvua kubwa kwenye baadhi ya maeneo, tunaiombea warudi kwenye majira ya joto,” amesema.

Amesema kabla ya hali ya hewa hiyo, walifanya maombi nchini kuombea mvua inyeshe nchini humo.

“Desemba 13, 2022 tulifanya maombi maalumu kuombea mvua nchini humo baada ya kulalamika hali ya ukame, Desemba 21, mvua kubwa ilinyesha na kusababisha maafa na bado wako kwenye kipindi hicho katika maeneo mengi.

“Sasa tunakwenda kuombea kubadili hali ya hewa nchini humo,” amesema Askofu Charles.

Akifafanua kwa nini Marekani na si nchi nyingine, Askofu Charles amesema hata nchi hiyo iliwahi kuisaidia nchi chakula ilipokuwa kwenye janga la njaa miaka ya nyuma.