Askofu Mkuu Ruzoka: Kardinali Rugambwa hana pa kwenda

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora, Paul Ruzoka

Muktasari:

  • Askofu Mkuu Paul Ruzoka awahakikishia waumini wa Jimbo Kuu la Tabora kuwa Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa kuendelea kubaki Tabora.

Tabora. Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora, Paul Ruzoka amesema kupata Ukardinali kwa Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa, ni tukio la pekee kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora na kwamba hana pa kwenda zaidi ya kubaki jimboni humo.

Askofu Mkuu Ruzoka ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya mapokezi ya Kardinali huyo iliyofanyika jimboni humo leo Jumamosi Oktoba 7, 2023 baada ya kuwasili akitokea Dar es Salaam.

Amesema kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiuliza baada ya kuwa Kardinali sasa ataenda wapi na kuwatoa wasiwasi waumini wa dhehebu hilo mkoani humo kuwa Mwadhama Protase Kardinali Rugabwa ataendelea kuwepo Jimbo Kuu la Tabora.

“...kwani ni jambo la kumshuru Mungu kwa tukio hili la kipekee wa wakazi wa Tabora ambapo miongoni mwao, ametokea Kardinali...baadhi ya watu wanauliza sasa anakwend wapi, hana pa kwenda,” amesema Askofu huyo huku waumini na wote waliohudhuria hafla hiyo wakishangilia, baada ya kuelezwa kuwa kardinali huyo ataendelea kuwepo jimboni humo.

Amesema Baba Mtakatifu ameona ni wakati wa kuwa na Kardinali mwingine ambaye safari hii anatoka Tabora na kwamba walikuwa jana na Mwadhama Polycalp Kardinali Pengo ambaye ndiye aliyempatia uaskofu wa Jimbo la Kigoma, Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa na sasa wote ni makardinali.