Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Asotea mafao kwa miaka 27

Muktasari:

  • Peter Kivike (62), anadai kusota kwa miaka 27 akidai mafao ya kuachishwa kazi, posho na nyongeza ya mshahara kama ilivyoelekezwa na kampuni ya Housing and Transport Pool ya Uholanzi aliyokuwa akiifanyia kazi.

Dar es Salaam. Peter Kivike (62), anadai kusota kwa miaka 27 akidai mafao ya kuachishwa kazi, posho na nyongeza ya mshahara kama ilivyoelekezwa na kampuni ya Housing and Transport Pool ya Uholanzi aliyokuwa akiifanyia kazi.

Kampuni hiyo iliyokuwa ni mradi wa maendeleo kati ya Tanzania na Uholanzi ilipunguza wafanyakazi wasiokuwa na uhitaji nao, Kivike akiwemo.

Kivike, ambaye ni mkazi wa Mabibo Dar es Salaam, alisema hakulipwa chochote ikiwa ni mafao ya kuachishwa kazi, posho na nyongeza ya mshahara kama ilivyoelekezwa na kampuni.

Akizungumza na gazeti hili, Kivike alisema kuwa kampuni hiyo iliyokuwa ni mradi wa maendeleo kati ya Tanzania na Uholanzi ilipunguza wafanyakazi na yeye akiwamo.

Baada ya kuachishwa kazi katika kampuni hiyo, Kivike alisema alipata ajira sehemu nyingine (hajaitaja), lakini mikosi iliendelea kumwandama, kwani siku moja alifuatwa na polisi kazini kwake wakidai kuna kifaa kilipotea kipindi anafanya kazi kwenye kampuni ya awali.

“Walinifuata mbele ya mwajiri wangu kwenye karakana yangu mpya wakiwa na polisi kutoka kituo cha Osterbay na baada ya vuta nikutuve kesi ikaisha kwa kuwa walikosa ushahidi wa hicho kifaa kilichopotea,” alisema.

“Nilifungua kesi kupinga kudhalilishwa mbele ya mwajiri wangu mpya nikidai fidia ya Sh5 milioni, lakini sijalipwa,” alisema.

Kivike alisema ilipofika Agosti 28, 2020, aliandika barua Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuomba msaada wa madai kwa mwajiri wa awali.

Alisema tangu ameanza kudai hajafanikiwa, hivyo kuomba msaada ikiwezekana aonane na Rais Samia Suluhu Hassan ili amesaidie.

“Nilishauriwa nitafute mwanasheria kwa ajili ya kuchanganua deni langu na nilifanya hivyo, nilitumia Sh500,000 mchanganuo ulionyesha nadai zaidi ya Sh77.51 milioni.

Alisema alipeleka barua Ubalozi wa Uholanzi nchini na alijulishwa kuwepo kwa deni hilo. Hata hivyo, Mei 12, 2021 alipata barua kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ikimueleza malalamiko yake yalipaswa kuwasilishwa kwenye kampuni ambayo kwa sasa haipo nchini.

“Wizara ikanishauri kusitisha madai yangu,” alisema.

Alisema kutokana na maelekezo hayo, Januari 24, 2022 aliamua kuandika barua kwenda Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kupata msaada zaidi, lakini hakufanikiwa.

Alipoulizwa Katibu Mkuu wizara hiyo, Joseph Sokoine, kuhusiana na suala hilo, alimwelekeza mwandishi kuzungumza na ofisa mwingine wizarani hapo.

“Kwa kumbukumbu zilizopo, Kivike alilipwa kila kitu mara baada ya kuachishwa kazi kwa maana hiyo hayo madai hayana msingi,” alisema ofisa huyo akikataa jina lake kuandikwa gazetini.

Kuhusu nyongeza ya mshahara alisema: “Kwenye suala la nyongeza ya mshahara, ubalozi ulisema utawaongeza watumishi wote waliokuwa wanafanya kazi kwenye ubalozi wa Uholanzi na sio wafanyakazi wa ule mradi aliokuwa akiufanyia kazi Kivike”.