Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Auawa akidai Sh6, 500

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilboad Mutafungwa akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 26, 2023. Picha na Anania Kajuni

Muktasari:

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu wa tatu wa familia moja kwa tuhuma za mauaji ya Peter Domini (48), Mkazi wa Kata ya Nyakabungo Wilaya ya Nyamagana mkoani humo.

Mwanza. Mkazi wa Kata ya Nyakabungo Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Peter Domini (48) ameuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani alipokwenda nyumbani kwa Julius Gaini (59) kudai Sh6,500 ya malipo ya pombe aliyomkopesha kilabuni kwake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 26, 2023, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema tayari wanawashikilia watu watatu wa familia moja wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo lililotokea Mei 25 mwaka huu Saa 2 usiku.

 “Peter Domini alifika nyumbani kwa Julius Gaini (59) mkazi wa Nyakabungo kwa nia ya kudai pesa yake Sh6,500 na baada ya kufika ulizuka ugomvi baina yao na kupelekea marehemu kushambuliwa,”

“Baada ya tukio hilo jeshi la polisi limefanya ufuatiliaji wa tukio hilo na kuwakamata Julius Gaini, Judith John (48) na Roda Julius (49) wakazi wa Nyakabungo kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Peter Domini, upelelezi katika tukio hili unaendelea na watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika,” amesema

Katika tukio lingine, jeshi hilo linawashikilia waganga wakienyeji 33 kwa madai ya kujihusisha na upigaji ramli chonganishi na kufanya shughuli za uganga wa kienyeji bila kufuata taratibu za kisheria.

Mutafungwa amesema katika oparesheni hiyo iliyofanyika kuanzia Mei 17  hadi 25, 2023 wamefanikiwa kukamata vielelezo mbalimbali ambavyo huvitumia kwenye shughuli zao.

“Nitoe wito kwa waganga wote wa kienyeji ambao wanafanya shughuliz hizo wafike katika ofisi za utamaduni ili kupata vibali vya kufanya shughuli hizo ili kupunguza matukio ya uharifu ambayo husababishwa na imani potofu,”amesema Mutafungwa