Auawa akituhumiwa kuwa mchawi
Muktasari:
- Mwalu Charles (45), mkazi wa kijiji cha Shilabela kata ya Ulewe wilayani Kahama mkoani Shinyanga amefariki kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana waliomtuhumu kuwa ni mchawi.
Shinyanga. Mwalu Charles (45), mkazi wa kijiji cha Shilabela kata ya Ulewe wilayani Kahama mkoani Shinyanga amefariki kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana waliomtuhumu kuwa ni mchawi.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Shinyanga, George Kyando amesema tukio hilo limetokea Septemba 9, 2021 katika kijiji cha Shilabela kata ya Ulewe tarafa ya Mweli Wilaya ya kipolisi Ushetu.
Amesema Mwalu (45) alikatwa mgongoni, kichwani na mkono wa kulia akibainisha kuwa chanzo ni mgogoro wa kifamilia unaotokana na imani za kishirikina, "marehemu alikuwa akituhumiwa kwa uchawi."