Baada ya Ndugai kujiuzulu, huu ndio mchakato

VIDEO: Baada ya Ndugai, huu ndio mchakato

Muktasari:

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amethibitisha kupokea barua ya aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai ikimtaarifu kujiuzulu nafasi hiyo na kusema utaratibu wa chama unaendelea wa kumpata Spika mwingine

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amethibitisha kupokea barua ya aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai ikimtaarifu kujiuzulu nafasi hiyo na kusema utaratibu wa chama unaendelea wa kumpata Spika mwingine.

Chongolo amesea hayo muda mfupi baada ya Ndugai kutoa taarifa akiutaarifu umma kuwa amejiuzulu nafasi hiyo na tayari ameshamuandikia barua mtendaji mkuu huyo wa CCM kumjulisha uamuzi aliouchukua.

Katika taarifa yake kwa umma, Ndugai alisema “Naomba kutoa taarifa kwa umma wa Watanzania kuwa leo tarehe 06 Januari 2022 nimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri wa wa Tanzania” ilisema taarifa ya Ndugai

Baada ya taarifa hiyo, Chongolo ameeleza kinachofuatia baada ya Ndugai kuachia ngazi akisema “Baada ya kuipokea barua hiyo jukumu langu ni kumjulisha Katibu wa Bunge kuhusu uwepo wa nafasi wazi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, zoezi ambalo linaendelea kwa utarajibu wa chama na baada ya hapo mchakato wa kumpata Spika mwingine utaendelea”