BREAKING NEWS: Spika Ndugai ajiuzulu

Muktasari:

Kwa mujibu wa barua aliyomuandikia Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema uamuzi huo ni wa kuachia nafasi hiyo ameufanya kwa hiari.


Dar es Salaam. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amejiuzulu nafasi hiyo leo Alhamisi Januari 6, 2022.

Kwa mujibu wa taarifa yake kwa umma, Ndugai amesema kuwa amemuandikia barua Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kujiuuzulu nafasi hiyo ikibainisha kuwa uamuzi huo wa kuachia nafasi hiyo ameufanya kwa hiari

“Naomba kutoa taarifa kwa uma wa watanzania kuwa leo Tarehe 06 Januari 2022 nimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri wa wa Tanzania” imesema sehemu ya taarifa hiyo nakuongeza

“Pia nakala yangu hiyo ya kujiuzulu nimewasilisha kwa katibu wa Bunge kwa ajili ya hatua stahiki kwa mujibu wa katiba ya nchi na sheria nyingine” amesema Ndugai kweneye taarifa yake kwa umma.

Ndugai ambaye ni mbunge wa Kongwa amesema anawashukuru  wabunge,  Rais Samia Suluhu Hassan, Serikali, wananchi wa Jimbo la Kongwa na Watanzania wote kwa ushirikiano waliompa kipindi akiwa Spika