Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baba mbaroni kwa kufanya mapenzi, kumpa ujauzito binti yake

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao

Muktasari:

Hamis Said (37), mkazi wa Mtaa wa Nkokoto mjini Igunga anashikiliwa na polisi kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kufanya mapenzi na kumpa ujauzito binti yake mwenye umri wa miaka 16.

Tabora. Hamis Said (37), mkazi wa Mtaa wa Nkokoto mjini Igunga anashikiliwa na polisi kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kufanya mapenzi na kumpa ujauzito binti yake mwenye umri wa miaka 16.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema binti huyo (jina linahifadhiwa) ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika moja ya shule za sekondari wilayani Igunga ambaye jina lake linahifadhiwa kutokana na umri wake.

"Tunamshikilia kwa mahojiano na tutamfikisha mahakamani mara baada ya upelelezi wa awali kukamilika,’’ alisema Kamanda Abwao

Bila kuelezea kwa kina tukio hilo lilivyogundulika hadi mtuhumiwa kutiwa mbaroni, Kamanda Abwao amesema kitendo hicho ni kinyume cha sheria na kinakiuka maadili, mila na desturi.

‘’Kitendo hiki kina taswira mbaya katika jamii na kinakiuka sheria inayokataza mahusiano ya kimapenzi kati ya wazazi na watoto wao au maharimu,’’ amesema Kamanda Abwao

Ameiomba jamii kukemea vitendo vya aina hiyo huku akiwasihi wenye taarifa za matukio ya namna hiyo kutoa taarifa kwa vyombo vya dola au viongozi wa Serikali katika maeneo yao kuwezesha hatua za kisheria dhidi ya wahusika.