Balozi Kamala afariki dunia

Muktasari:

  • Amefariki dunia jijini Dar es Salaam katika Hospital ya Mzena alipokuwa akipatiwa matibabu.

Dar es Salaam. Aliyewahi kuwa mbunge wa Nkenge na Waziri wa Afrika Mashariki, Dk Diodorus Kamala, amefariki dunia leo Februari 12, 2024 katika Hospital ya Mzena jijini hapa alipokuwa akipatiwa matibabu.

 Akizungumza na Mwananchi, dada wa Marehemu, Ritha Kamala, amesema”

"Ni kweli amefariki majira ya saa moja jioni katika hospitali ya Mzena alipokuwa akipatiwa matibabu," amesema dada huyo wa marehemu bila kutoa taarifa za kina kuhusu ugonjwa wake.

Dk Kamala aliyezaliwa Novemba 26, 1968 alikuwa mbunge wa Nkenge kuanzia mwaka 2000 hadi 2010 na mwaka 2006 aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Afrika Mashariki na baadaye Waziri Kamili mwaka 2008 hadi 2010

Mwaka 2011 aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Uholanzi ambako alitumikia nafasi hiyo hadi mwaka 2015 aliporejea kuwa mbunge hadi mwaka 2020.