Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bashungwa kulivalia njuga deni Temesa

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (katikati), Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) Lazaro Kilahala (Kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Aisha Amour mara baada ya kutembelea Temesa.

Muktasari:

  • Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameahidi kushughulikia deni la Wakala wa Ufundi na Umeme (Tamesa) wanaodai kwa taasisi mbalimbali nchini huku akitoa maagizo kwa wakala huyo kubadilika kifikra.

Dodoma. Wakala wa Ufundi na Umeme (Tamesa) unazidai taasisi mbalimbali Sh32.5 bilioni kutokana na huduma walizopatiwa kupitia wakala huo.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Septemba 6, 2023 na waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa alipotembelea wakala huo jijini Dodoma.

Hiyo ni ziara ya kwanza kwa Bashungwa tangu ateuliwe Agosti 30, 2023 na Rais Samia Suluhu Hassan kuongoza wizara hiyo mpya iliyotokana na kugawanywa kwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.

“Nimekubaliana na Temesa baadhi ya vitu vya kufanya kazi na nitaomba kikao na Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba kujadili madeni hayo kwa kuomba Hazina wawasaidie malipo hayo yalipwe ili mikakati ya kuwezesha wakala hiyo kuwa bora yafanyike,” amesema.

Amesema hadi hivi sasa Temesa inadai madeni ambayo yamehakikiwa na Hazina ya Sh32.5 bilioni.

Aidh, Bashungwa amesema ametoa miongozo na kutaka aanze kuona matokeo yake ndani ya miezi mitatu.

Amesema pamoja na kazi nzuri inayofanyika na Temesa lakini kumekuwa na changamoto kwenye upande wa utengenezaji wa magari ya Serikali na mitambo.

Hata hivyo, amesema kwa namna ambavyo Temesa ilivyoundwa na dhamira na malengo yake bado ni taasisi muhimu na dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha inakuwa taasisi bora inayotoa huduma bora kwa Watanzania.

Bashungwa amesema hadi kufikia Juni mwaka 2023, Serikali ilikuwa imetoa Sh112 bilioni kama ruzuku kwa wakala huo.

Amewaomba wadau watakaokuja kupata huduma waendelee kuwa na imani kwamba watakuja kufanya mabadiliko makubwa ambayo yatafanya Temesa iwe taasisi kubwa inayotoa huduma bora.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Temesa, Lazaro Kilahala amesema wamepokea maelekezo ya Serikali yanayotaka kuona wanakuwa wa kisasa zaidi, kujiendesha kwa ufanisi na tija na watayafanyia kazi.