Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bavicha yawaita vijana kushiriki wiki ya maandamano

Muktasari:

  • Baraza la Vijana la Chadema, limewaomba vijana nchini kujitokeza katika wiki ya maandamano yatakayoanza Aprili 22 hadi 30 yanayolenga kuishinikiza Serikali kushughulikia changamoto ya gharama za maisha.

Dar es Salaam. Baraza la Vijana Chadema  (Bavicha) limesema lipo tayari kwa ajili ya wiki ya maandamano ya amani itakayoanza Aprili 22 hadi 30 ikiwa ni utekelezaji wa azimio la Mtwara la chama hicho kikuu cha upinzani.

Machi 6, 2024 viongozi wakuu wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe walijifungia mkoani Mtwara na kutoka na azimio la maandamano yatakayofanyika katika kila makao ya makuu ya mikoa nchi nzima.

Hatua hiyo imekuja baada ya chama hicho kufanya maandamano yaliyopewa jina la vuguvugu la haki kwa lengo la kushinikiza Serikali kushughulikia kupanda kwa gharama za maisha, kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu miswada mitatu ya sheria ya uchaguzi ambayo imeshakuwa sheria baada ya Rais Samia Suluhu Samia kuisaini hivi karibuni.

Leo Ijumaa Aprili 5, 2024 akizungumza na wanahabari Mwenyekiti wa Bavicha, John Pambalu amesema baraza hilo lipo tayari kwa ajili ya maandamano hayo, huku likitoa wito kwa vijana wengine kuungana nao katika wiki ya mchakato ili kufikisha ujumbe wa kilio cha gharama za maisha.

Katika mkutano huo Pambalu amesema tangu Rais Samia aingie madaraka gharama za maisha zimekuwa juu na kusababisha baadhi ya Watanzania kushindwa kuzidumu kutokana na kuwa na kipato kidogo kisichotosha kukidhi mahitaji ya kila siku.

"Maisha yamekuwa magumu hayawapumzishi Watanzania yanawataabisha kwa sababu ya mfumuko wa bei, licha ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kusema mfumuko wa bei umepungua, " amesema Pambalu.

Aprili 3, 2024 akiwasilisha hotuba ya makadirio ya bajeti ya ofisi yake, Majaliwa alisema katika kipindi cha Julai hadi Disemba 2023, wastani wa mfumuko wa bei umepungua na kufikia asilimia 3.2 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 4.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2022.

Hata hivyo, Pambalu amedai Bavicha hawakubaliana na maelezo hayo ya Majaliwa kwa kuwa bado bidhaa za muhimu ikiwemo sukari, mafuta ya petroli bei zake zipo juu ukilinganisha na awamu iliyopita.

Mbali na hilo, Pambalu amesema maandamano hayo yana lengo pia la kupinga hatua ya Rais Samia kusaini miswada mitatu ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi na Sheria ya Vyama vya Siasa.

"Tunapinga hatua ya Rais Samia kusaini miswada hiyo na kuwa sheria licha ya kuwepo kwa kelele nyingi za wadau waliotaka kiongozi huyo asisaini hadi mabadiliko ya kikatiba yafanyike kwanza lakini imeshasainiwa kinyume na matarajio ya wengi,” amesema.

Ameongeza kuwa "Tunatoa wito kwa vijana wenzetu kuunga mkono azimio la chama la Mtwara pia kulaani hatua ya Rais Samia kusainiwa miswada hii, narudia tunawaomba vijana wa mikoa mbalimbali kujitokeza kwenye maandamano haya."

Pambalu amefafanua kuwa vijana wa Tanzania wakiwemo waendesha pikipiki, mama lishe, mafundi gereji, wana sababu za kushiriki maandamano kutokana kilio cha gharama za maisha yanayowakumbuka.