Benki ya Exim yang’ara tuzo za NBAA

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania, Jaffari Matundu amepokea tuzo kwa niaba ya benki hiyo toka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Jamal Kassim baada ya benki kuwa miongoni mwa benki tatu bora katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2021 (Best Presented Financial Statements for the Year 2021 Awards) zinayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA).

Tuzo hizo zilitolewa jijini Dar es Salaam hivi karibuni zimeshuhudiwa na Mwenyekiti Bodi ya NBAA, CPA Prof. Sylivia Shayo.

Mwakilishi kutoka Benki ya Exim Tanzania,  Frim Paul (Kulia) akipokea tuzo kwa niaba ya benki hiyo toka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Jamal Kassim ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa benki hiyo


katika kufanikisha maandalizi ya tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2010 (Best Presented Financial Statements for the Year 2021 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA). Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa  NBAA, CPA Pius Maneno.

Viongozi waandamizi wa Benki ya Exim Tanzania wakiongozwa na Jaffari Matundu  (katikati)  wakionesha tuzo  walizopata

kwenye hafla ya  tuzo za umahiri katika uandaaji wa taarifa za Fedha ya Mwaka 2010 (Best Presented Financial Statements for the Year 2021 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).


Muonekano wa tuzo umahiri ambazo benki ya Exim Tanzania ilifanikiwa kuzitwaa kwa wakati wa hafla ya  tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2010

(Best Presented Financial Statements for the Year 2021 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).


Washindi wa  tuzo mbalimbali  zilizotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu wakati wa utoaji wa tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2021 (Best Presented Financial Statements for the Year 2021 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.