Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bodaboda wadaiwa kumuua, kumchoma moto anayedaiwa kushiriki kuiba pikipiki

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), George Katabazi

Muktasari:

  • Mtu huyo alikamatwa na madereva bodaboda baada ya wenzake kutoroka, kisha kuchomwa moto.

Babati. Mwanaume anayekadiriwa kuwa na miaka 21, ameuawa na kundi la waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda katika Mtaa wa Wang'waray mjini Babati mkoani Manyara.

Mtu huyo ameuawa akidaiwa kushirikiana na wenzake wawili kuiba pikipiki.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, George Katabazi, akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Julai 2, 2024 ofisi yake mjini Babati, amesema tukio hilo limetokea jana Julai mosi, 2024 saa sita mchana katika  mtaa wa Wang'waray mjini Babati.

Amesema mtu huyo ameuawa baada ya kudaiwa kushiriki kupora pikipiki, akiwa na wenzake wawili.

Amesema kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mtu huyo alikuwa abiria wa pikipiki na alikuwa akiwasiliana na wenzake kabla ya kupora pikipiki hiyo.

"Indaiwa kuna viashiria alikuwa anawasiliana na wenzake na alimpitisha kwenye njia waliyokuwepo wenzake na wakapora pikipiki, kisha wakatokomea kusipojulikana," amedai Kamanda Katabazi.

Amedai baada ya wenzake kupora pikipiki hiyo na kutokomea, dereva wa pikiki hiyo alipiga kelele na watu waliokuwa karibu walikwenda kumsaidia kumkamata aliyebaki.

Amesema baada ya kukamatwa mtu huyo, kundi hilo la watu wanaodaiwa ni madereva bodaboda wa eneo hilo walidai wanampeleka kituo cha Polisi, lakini hawakufanya hivyo na badala yake walimwagia petroli na kumchoma moto.

"Hadi hivi sasa bado haijabainika, marehemu ni nani na ametokea maeneo gani, ila polisi tunaendelea na uchunguzi wa tukio hili," amesema Kamanda Katabazi.

Hata hivyo, shuhuda wa tukio hilo, Joanes Bura amedai simu ya mtu huyo aliyeuawa ilipopekuliwa ilikutwa na mawasiliano ya wezi wenzake.

"Mtu huyo kabla ya kifo chake alikuwa anawasiliana kwa ujumbe mfupi wa simu kuwa amsogeze mwenye pikipiki maeneo waliyokuwepo wenzake," amedai shuhuda huyo.

Amesema wenzake wawili wamefanikiwa kukimbia, ila yeye alishindwa na kuishia kuchomwa moto.