Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Buriani Mzee Simama, mtunzi wimbo wa JWTZ, ‘ni mimi mwanajeshi’

Muktasari:

  • Safari ya Mzee Simama jeshini ilianza mwaka 1979 alipopata mafunzo ya awali ya kijeshi katika Kikosi cha Jeshi 815 KJ. Alisajiliwa rasmi kuwa mwanajeshi wa JWTZ mwaka 1984 akipewa namba ya utumishi MT 54333.

Dar es Salaam. Safari ya mwisho ya askari mstaafu wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ), (WO II) Celestine Koromba Simama, imehitimishwa Juni 16, 2026 katika mazishi yaliyofanyika katikaa makaburi ya Toangoma, Kongowe jijini Dar es Salaam, akiacha alama katika sanaa ya muziki uliotumika jeshini.

Askari huyo aliyestaafu mwaka 2014, alifariki dunia alfajiri ya Juni 12, 2026, akiwa anapatiwa matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) baada ya kupata ajali ya barabarani mwishoni mwa Mei 2026.

Askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ wakitoa heshima za mwisho kwa askari mstaafu wa jeshi hilo Celestine Simama, Juni 16, 2026 katika mazishi yaliyofanyika makaburi ya Toangoma Kongowe Dar es Salaam.

Moja ya alama isiyofutika aliyoiacha Mzee Simama ni wimbo maarufu jeshini "Ni mimi mwanajeshi."

Mzee Simama ni nguli wa muziki wa mapipa au ‘Steel pan’ ambao hutengenezwa kwa mapipa ya chuma yaliyotumika kuhifadhia mafuta. Sehemu ya juu ya pipa kutengenezwa kwa ustadi na hupigwa kwa kutumia vijiti maalumu.

Akieleza chanzo cha kifo cha baba yake, mtoto wa marehemu Agatha Koromba amesema mauti yalianza kumnyemelea Mei 29, 2026, alipopata ajali ya barabarani.

“Aliwahishwa kwa matibabu ya dharura katika Hospitali ya Polisi Kilwa Road na baadaye kupewa rufaa kwenda MOI. Ingawa madaktari na wauguzi walipambana usiku na mchana kuokoa maisha yake, Juni 12, 2026, saa 11:00 alfajiri baba akafariki,” amesema

Akieleza zaidi amesema baba yake alikuwa kioo kwa vijana walio wengi kwa kutumia mziki wa mapipa kuwalea, kuwafundisha nidhamu na kuwapa fursa ya kukuza vipaji vyao.

Waombolezaji wakimuaga aliyekuwa askari mstaafu wa jeshi la JWTZ, Celestine Simama, wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika Juni 16, 2026 Kongowe, Dar es Salaam.

“Baba alipenda sana nidhamu,” aliongeza Agatha siku ya mazishi.

Sebastian Francis mmoja ya wanafunzi wa mziki wa mapipa wa Mzee Simama amesema alitamani sana mziki huo uthaminiwe zaidi nchini.


Chimbuko lake

Mzee Simama alizaliwa Mei 19, 1958, Kijiji cha Nyegina, Wilaya ya Musoma Vijijini, mkoani Mara. Alikuwa mtoto wa pili kati ya watoto 16 wa familia ya Nicephori Simama na Theresia Obule.

Akiwa mtoto aliyelelewa katika misingi ya Kikristo, alipata sakramenti ya Ubatizo mwaka huo huo wa 1958 katika Parokia ya Koaki, Kata ya Nyatorogo na baadaye akakomazwa katika imani kwa kupokea sakramenti ya Kipaimara.


Safari ya elimu

Kiu yake ya elimu ilianzia katika Shule ya Msingi Mwisenge, ambapo alihitimu mwaka 1973. Baadaye alichaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari Tarime-Rorya mkoani Mara kwa elimu ya sekondari.

Askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ wakitoa heshima za mwisho kwa askari mstaafu wa jeshi hilo Celestine Simama, Juni 16, 2026 katika mazishi yaliyofanyika makaburi ya Toangoma Kongowe Dar es Salaam.

Hakushishia hapo, alielekea jijini Dar es Salaam na kujiunga na Shule ya Sekondari Jitegemee kwa ajili ya masomo ya Kidato cha Tano na Sita.


Ndani ya kombati miaka 30

Safari ya Mzee Simama jeshini ilianza mwaka 1979 alipopata mafunzo ya awali ya kijeshi katika Kikosi cha Jeshi 815 KJ. Alisajiliwa rasmi kuwa mwanajeshi wa JWTZ mwaka 1984 akipewa namba ya utumishi MT 54333.

Katika utumishi wake uliotukuka kwa zaidi ya miongo mitatu, alihudumu katika vikosi mbalimbali ikiwemo 815 KJ, 822 KJ Rwamkoma na Shule ya Kijeshi ya Muziki (Band Coy- Mwenge).

Nidhamu, uaminifu na bidii yake vilimfanya apande vyeo hatua kwa hatua hadi kufikia cheo cha Warrant Officer Class II (WO II), kabla ya kustaafu kwa heshima zote mwaka 2014.

Mbali na kuwa askari hodari, Mzee Simama alikuwa na kipaji cha kipekee cha muziki. Serikali na jeshi vilitambua kipaji chake na kumtuma nchini Guyana, Amerika ya Kusini, ambako alihitimu Stashahada ya Muziki wa Mapipa na Utengenezaji wa Ala za Muziki.

Miongoni mwa mambo makubwa yatakayomfanya akumbukwe daima ni wimbo "Ni mimi Mwanajeshi", alioutunga akiwa Band Coy-Mwenge.

Aidha, Ndiye mwanzilishi wa bendi ya muziki wa mapipa (Steel Band) katika Kikosi cha Jeshi 831 KJ.


Ualimu na malezi

Alifundisha muziki katika Chuo cha Tangaza nchini Kenya, Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST), Makongo, Southern Highlands na Shule ya Sekondari Jitegemee ambako pia alitunga wimbo rasmi wa shule hiyo.

Pia alijitolea kulea vijana kiroho na kisanaa katika vituo vya Salesian Don Bosco Temeke na Oysterbay.


Ndoa na familia

Mwaka 1990, Mzee Simama alifunga ndoa na Sabina Kubuke katika Parokia ya Chang'ombe, Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Ndoa yao ilibarikiwa kupata watoto wawili Agatha na Cassian. Alikuwa mume na baba mfano wa kuigwa aliyetunza na kusimamia maadili ya familia yake.