Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CCM Kilimanjaro yampongeza Rais Samia

Muktasari:

  • Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro kimetoa tamko rasmi la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha za maendeleo zaidi ya Sh17 bilioni.

  


Rombo. Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro kimetoa tamko rasmi la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha za maendeleo zaidi ya Sh17 bilioni.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Rombo, Mwenyekiti wa chama hicho wilayani humo, Antony Tesha amesema fedha hizo za maendeleo zilizotolewa zimeweka historia katika wilaya hiyo kwani haijawahi kutokea.

"Tunaishukuru serikali yetu inayoongozwa na Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha kiasi cha zaidi ya Sh17 bilioni kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hasa kwenye sekta ya elimu, afya, barabara, maji hakika ni faraja kubwa sana kwetu sisi wana Rombo.

"Jambo hili halijawahi kutokea katika historia ya wilaya hii ya Rombo,hivyo basi tuna kila sababu ya kumpongeza Rais Samia ,ametutendea makubwa katika wilaya hiyo ya Rombo,"amesema Tesha

Naye Mwenyekiti wa chama hicho, Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi amesema serikali ya awamu ya sita itaendelea kutekeleza ilani ya chama hicho na wao wataendelea kutembea hatua kwa hatua na Rais Samia ili yale yaliyoahidiwa ndani ya ilani ya chama hicho yanatekelezwa kikamilifu.