Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chadema Njombe walia viongozi wao kubambikiwa kesi za mauaji


Muktasari:

  • Mwenyekiti Chadema mkoa wa Njombe alia na utawala wa mabavu ulivyowafanya viongozi wao kupewa kesi ya mauaji.

Njombe. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Njombe, Rose Mayemba amesema siasa za mabavu katika utawala uliopita hazikukiacha salama chama hicho baada ya viongozi wao kukamatwa kwa kupewa kesi ya mauaji.

Hayo ameyasema leo Jumatatu mbele ya mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Stendi ya Zamani hapa mkoani Njombe.

Amesema mwaka 2020 wakati wa uchaguzi mkuu vijana wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Njombe pamoja na vijana wengine watatu walikamatwa na kupewa kesi ya mauaji.

Amesema mpaka sasa vijana hao wapo gerezani kwa kipindi cha miaka miwili sasa na hawajui hatima ya maisha yao kutokana na kesi hiyo.

"Mheshimiwa mwenyekiti mimi ninafahamu kwamba vikao vya maridhiano vinaendelea kwa ushawishi wako tunakuomba vijana wale nao wawe pia huru," amesema Mayemba.

Amesema vijana hao wana haki ya kupata kile ambacho wanakipata wengine kwasababu hakuna asiyejua kuwa kesi hiyo msingi wake ni siasa.

Amesema lengo kubwa ilikuwa kukinyima chama hicho uhalali wa kuchaguliwa katika kipindi cha uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2020.

Baadhi ya wanachama wa chama hicho wakiwemo Bartan Sanga na Elizabeth Ngimbudzi wamesema ujio wa mwenyekiti wa chama hicho Taifa utasaidia kutatua changamoto zilizokuwa zinawakabili vijana ikiwemo kukamatwa kwa viongozi wao.

"Kuna ndugu zetu wapo mahabusu na toka wafungwe mpaka sasa hatujui kinachoendelea kwahiyo kupitia kiongozi wetu itakuwa rahisi kuzungumza na viongozi wenzie," amesema Sanga.