Chadema wataka wananchi kuendelea kujikinga na magonjwa ya mlipuko

Muktasari:

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewataka Watanzania kuendelea kujikinga na kuchukua tahdhari zinazotolewa na wataaalamu wa afya dhidi ya magonjwa yanayoambukiza ikiwemo corona.

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewataka Watanzania kuendelea kujikinga na kuchukua tahdhari zinazotolewa na wataaalamu wa afya dhidi ya magonjwa yanayoambukiza ikiwemo corona.

Wito huo umetoleawa ikiwa ni siku chache tangu Serikali kupitia Wizara ya Afya kuagiza wananchi kujikinga na magonjwa yanayoambukiza ikiwemo Corona.

Februari 23, 2021 Waziri wa Afya Dk, Dorothy Gwajima akiwa jijini Dodoma alitoa tamko la kuongezeka kwa kasi ya utekelezaji wa wa hatua ya kujikinga na magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambuakiza.

Akizungumza na wanahabari leo Ijumaa Machi 5, 2021 Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amesema Watanzania wanapaswa kujikinga na kuchukua kila tahadhari zinazotolewa na wataalamu wa afya.

"Tunapaswa kuendelea kuchukua kila tahadhari ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa, kunawa mara kwa mara na maji tiririka na sabuni pamoja na kuepuka misongamano ikiwemo kukaa umbali wa mita moja," amesema Mnyika.

"Serikali, itekeleze zoezi la upimaji na utoaji wa takwimu na kufungua milango kwa taasasi nyingine kwani sampuli zinaweza kuchukuliwa popote," amesema

Pia, Mnyika amesema kutokutoa taarifa na takwimu kunaweza kupelekea wananchi kutochukua tahadhari jambo linalowezamkuongeza kasi ya maambukizi.