Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chongolo: Kipaumbele chetu ni afya ya mama na mtoto

Mbulu. Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amesema chama chake kimeweka msisitizo kwenye afya ya uzazi ya mama na mtoto ili kupunguza vifo hivyo kwa asilimia 100.

Chongolo amebainisha hayo leo Machi 6, 2023 wilayani Mbulu mkoani Manyara wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020 ambapo ametembelea miradi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa vituo vya afya.

Akiwa Mbulu, Chongolo ametembelea kituo cha afya ya mama na mtoto cha Haidom na kueleza kwamba ujenzi wa kituo hicho ni moja ya utekelezaji wa ahadi za chama hicho katika kuimarisha afya ya mama na mtoto.

"Serikali imejizatiti kutoa huduma bora za afya na kipaumbele chetu ni afya ya uzazi ya mama na mtoto. Mama zetu wamekuwa wakipata changamoto za uzazi kwa sababu ya umbali wa vituo vya afya.


"Tumeamua kujenga vituo vya afya kila mahali na lengo letu ni kukomesha vifo vya mama na mtoto kwa asilimia 100. Kila tunakopita tunasisitiza utekelezaji wa maagizo ya chama katika eneo hilo," amesema kiongozi huyo.

Chongolo amebainisha pia kwamba mbali na huduma za mama na mtoto, wanasimamia uboreshaji wa huduma za afya kwa watu wengi kwa kujenga wodi za wanaume, watoto na majengo ya kuhifadhia maiti.

"Serikali ina wajibu wa kuwalinda wananchi, mali zao, afya zao na haki zao. Hayo ni maelekezo ya CCM na serikali inayatekeleza kikamilifu," amesema Chongolo ambaye pia ametembelea shina namba 4 lililopo katika Kijiji cha Haidereli.

Kwa upande wake, Katibu wa Organaizesheni wa CCM, Issa Haji Gavu amewahimisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo na za kichama ili kuisimamia serikali yao.

"Serikali yenu inawaletea maendeleo hadi vijijini, endeleeni kushirikiana na viongozi wenu katika kujiletea maendeleo. Nawapongeza kwa kujibidiisha kwenu kwenye shughuli za maendeleo," amesema Gavu.