Chongolo: Viongozi wa dini, waumini ombeeni Taifa
Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo akizungumza katika ibada ya kanisa la EAGT la Mafinga, Wilayani Mufindi
Muktasari:
- Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amewakumbusha viongozi wa dini na waumini umuhimu wa kuliombea Taifa ili amani na utulivu vilivyopo viendelee kudumu.
Mufindi. Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amewaomba viongozi wa dini na waumini kuliombea Taifa ili amani na utulivu viliyopo viendelee kudumu.
Chongolo amesema hayo leo Jumapili Mei 28, 2023 baada ya kuhudhuria ibada ya Jumapili katika kanisa la EAGT, Mafinga mjini.
"Endeleeni kuombea Taifa, tusipoombea Taifa hili tutakuwa hatujatimiza wajibu wetu," amesema Chongolo.
Amewaambia waumini wa kanisa hilo kuwa lengo la ziara yake ni kupita kwenye miradi kuona namna utekelezaji wa miradi inavyoendelea. Nia ya Serikali ni kutatua changamoto za wananchi," amesema Chongolo.
Chongolo ambaye alikabidhi Sh2 milioni kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan ili kumalizia ujenzi wa kanisa hilo.
"Rais Samia anawasalimia sana na ametoa hizi hela baada ya kumwambia nitakuja, nilichangia ujenzi wa kanisa awali na sasa pokeeni fedha hizi," amesema Chongolo.
"Tuliahidi na lazima tutekeleze, tumekuja kuona namna ilanibinatekelezwa,"alisema.
Awali, Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa CCM, Sophia Mjema amewakumbusha wazazi kuhusu malezi ya watoto.
"Isipite masaa mawili hujamuombea mtoto wako, hakikisheni mnakuwa karibu na watoto. Jua anakaa na nani, rafiki yake nani na anaongozana na nani," amesema.
Mchungaji wa kanisa hilo, Walezi Wahoa amesema wataendelea kuombea Taifa kila wanapofanya maombi.