Chuo cha Usafiri wa Anga na Pro Wings watoa mafunzo ya kurusha drone Arusha

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

Chuo cha Usafiri wa Anga nchini (CATC) kwa kushirikiana na Chuo cha Pro Wings cha  Afrika Kusini kimeanza kutoa mafunzo ya kurusha ndege zisizo na rubani kwa muda wa wiki nne yanayofanyika katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela (NM-AIST).

Arusha. Chuo cha Usafiri wa Anga nchini (CATC) kwa kushirikiana na Chuo cha Pro Wings cha  Afrika Kusini kimeanza kutoa mafunzo ya kurusha ndege zisizo na rubani kwa muda wa wiki nne yanayofanyika katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela (NM-AIST).
Akifungua mafunzo hayo Makamu Mkuu wa Chuo cha NM-AIST, Profesa Emmanuel Luoga amesema  ni muhimu kwa taasisi hiyo kuwawezesha wakufunzi kutumia ndege zisizo na rubani (drone) katika shughuli za tafiti mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo sanjari na kuendeleza teknolojia.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Amesema kutokana na kukua kwa maendeleo ya teknolojia duniani katika miaka ya hivi karibuni matumizi ya drone yameendelea kuongezeka na kutumika kwenye shughuli za kijeshi na raia hivyo kuwapa watumishi mafunzo ni sehemu ya kuhakikisha usalama wakati wa matumizi yake.
“Matumizi ya ndege zisizo na rubani yamekua yakifanyika kwenye shughuli za michezo,mikusanyiko ya aina mbalimbali na kifaa muhimu kwa wapigapicha za kibiashara,tafiti za kilimo na shughuli zingine,”amesema Profesa Luoga