Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DC Arumeru atoa siku saba wananchi kung'oa bangi shambani

Mkuu wa wilaya Arumeru Emmanuela Kaganda akionesha bangi iliyovunwa na kuhifadhiwa kwenye masufuria Kijiji Cha Kisimiri juu.

Arusha. Wananchi wa Kijiji cha kisimiri Juu wilaya ya Arumeru wamepewa siku saba kung'oa miche ya bangi katika mashamba yao baada ya kubainika kuendelea na kilimo hicho licha ya kupigwa marufuku.

Kubainika kwa mashamba hayo katika Kijiji hicho kumetokana na operesheni iliyofanywa na kamati ya ulinzi na usalama katika wilaya hiyo kwa kushirikiana na baadhi ya Wananchi iliyofanyika June 11, 2023 na kufanikiwa kung’oa hekari 60 za zao hilo.

Maagizo hayo yamekuja takriban siku tatu tangu operesheni nyingine iliyofanywa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya (DCEA) iliyoongozwa na Kamishna Jenerali Aretas Lyimo katika vijiji vya Arumeru ambapo gunia 931 za Bangi zilikamatwa Arumeru.

Katika operesheni hiyo iliyofanyika kijiji cha Lesinoni na maeneo ya jirani pia hekari 953 za bangi ziliteketezwa na ilibainika uwepo wa bangi mbichi gunia 4,975 na watu 16 walikamatwa.

Mkuu wa Wilaya  ya  Arumeru  Emmanuela  Kaganda akizungumza wakati wa   operesheni  Kijiji Cha Kisimiri ameonya baadhi ya wananchi kuendelea kwa Kilimo hicho na kutoa siku Saba kung'oa bangi mashambani.

"Baada ya siku saba tutafanya opesheni kubwa mashambani na ambao mashamba yao yatakutwa na bangi hatua kali za kisheria zitachukuliwa,"amesema.

Amesema katika operesheni  hiyo  wamefanikiwa  kukamata gunia 10 za bangi  kavu, kukusanya  mbegu  za bangi  kg 30 na kuteketeza  hekari  60 za mashamba  ya  bangi  mbichi.

Mwenyekiti  wa  kijiji hicho, Mayani Lukumay  ameiomba Serikali  kuboresha  miundombinu  ya  barabara  kufika kijijini hapo kwani wananchi wanaweza kulima mazao mengi.

"Eneo hili tunaweza kupata mavuno makubwa Kama tukiongeza nguvu katika kilimo cha viazi, njegere,pareto lakini changamoto  kubwa ni namna ya kuyafikisha mazao  hayo sokoni,"amesema.