Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DC Moshi awaonya wananchi waliotaka kuvuruga mradi wa maji

New Content Item (2)
New Content Item (2)

Muktasari:

Mkuu wa Wilaya ya Moshi (DC), Abbas Kayanda ametoa onyo kwa wananchi wa kijiji cha Mowo Kata ya Kimochi wilayani humo ambao walitaka kupinga na kuvuruga mradi wa maji unaotekelezwa kwa fedha za Serikali zaidi ya Sh900 milioni kwa madai ya kutoshirikishwa mradi huo.

Moshi. Mkuu wa Wilaya ya Moshi (DC), Abbas Kayanda ametoa onyo kwa wananchi wa kijiji cha Mowo Kata ya Kimochi wilayani humo ambao walitaka kupinga na kuvuruga mradi wa maji unaotekelezwa kwa fedha za Serikali zaidi ya Sh900 milioni kwa madai ya kutoshirikishwa mradi huo.

Amesema hatawafumbia macho wananchi watakaoharibu miundo mbinu hiyo ya maji na watakaozuia kutekelezwa kwa mradi huo na kusema ni lazima miundo mbinu ya maji iboreshwe ili wananchi waweze kupata maji ya uhakika.

Kayanda ametoa onyo hilo leo Ijumaa Juni 3, 2022 wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Kimochi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mowo ambacho mradi huo wa maji unatekelezwa.

"Maji ni rasilimali ya umma na ndio maana sehemu zote maji yanasimamiwa na Serikali na sio kikundi cha watu, sisi watendaji tunawajibu wa kuusimamia na sio kupinga, tunataka kuboresha miundo mbinu ili maji haya yaweze kuwanufaisha watu wengi kuliko ilivyokuwa sasahivi,"

"Na huo ndio utaratibu, hilo ni lazima mlielewe ndugu zangu na wala tusifanye mambo kwa ushabiki, Serikali imeleta fedha ili tuboreshe mundo mbinu ya maji ili maji yapatikane vizuri na kwa utoshelevu," amesema Kayanda na kuongeza

"Nataka niwaambie kijiji chenu hiki kina tabia ya kupinga zoezi hili ambalo linatekelezwa na Serikali sasa niwaambie sheria inasema yoyote yule atakayezuia utekelezaji wa mradi wa maji adhabu yake ni faini kuanzia Sh5 milioni hadi Sh50 milioni au kifungo cha miaka miwili au vyote viwili kwa pamoja,"

"Nawaambieni kama kuna mtu anafikiri Serikali inatania katika suala hili la miundo mbinu ya maji nendeni mkaharibu, wajumbe wa Serikali wa kijiji mpo hapa na dhamana yenu kubwa ni kulinda miundo mbinu hii iliyopo, ikiharibiwa nyie wote mtawajibika kwa namna moja au nyingine kwa mujibu wa sheria za nchi," amesema Kayanda

"Natoa onyo kali msifanye mzaha na hizi rasilimali ambazo Serikali imeleta hapa kila mtu ana wajibu wa kuilinda na kuitunza kwasababu sio kwa manufaa yetu sisi tuu ni pamoja na vizazi vyetu, hivyo tusidanganyane katika mazingira haya,"amesema

Pamoja na mambo mengine, Kayanda amewatoa hofu wananchi wa kata hiyo na kuiagiza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi (MUWSA) ambayo ndio wanaosimamia mradi huo kuhakikisha vijana wa eneo hilo wanapata ajira zinazotokana na utekelezwaji wa mradi huo.

Mkurugenzi wa maji MUWSA, Kija Limbe amesema mradi huo wa maji unaotekelezwa kwa fedha za Serikali ulipelekwa katika kata hiyo kutokana na changamoyo kubwa ya maji iliyokuwepo kwa wananchi wa ukanda wa tambarare ambapo mradi huo utagharimu zaidi ya Sh900 milioni.

"Mradi huu umekuja hapa baada ya kuona eneo ambalo ni la ukanda wa chini katika kata hii ya Kimochi wanachangamoto kubwa ya maji, lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma ya maji safi na salama,"amesema Limbe

Awali wananchi wa kijiji hicho, Witness Kalalu na Awinia Kitiwi wamesema hawapingi mradi huo wa maji kuwepo bali ni kuwa hawajashirikishwa kikamilifu kuhusu mradi huo na kwamba vijana wanaozunguka mradi huo wa maji hawajapewa kipaumbele cha ajira.