Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dereva wa lori lililoua watano Kilimanjaro mbaroni

Muktasari:

  • Ajali hiyo ambayo  ilitokea jana Jumapili katika Barabara ya Mwika-Himo  katika eneo la Coca cola Riata, Kata ya Mwika kusini, Wilaya ya Moshi, ilisababisha vifo vya watu watano na wanne kujeruhiwa.

Moshi. Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia dereva wa gari aina ya Scania iliyokuwa imebeba shehena ya maji tani 30, Elias Uledi (46) mkazi wa Kisongo kwa kusababisha ajali iliyoua watu wa tano na kujeruhi wanne mkoani Kilimanjaro.

Ajali hiyo ilitokea jana katika Barabara ya Mwika-Himo  katika eneo la Coca Cola Riata, Kata ya Mwika kusini, Wilaya ya Moshi baada ya gari hilo kuligonga kwa nyuma gari la abiria aina ya Toyota Noah na kuiburuza mita kadhaa kisha kupinduka na kuilalia na kusababisha vifo na majeruhi.
Akizungumzia kukamatwa kwa dereva huyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema chanzo cha ajali hiyo ni kutokana na uzembe wa dereva wa gari hilo la maji kushindwa kulimudu gari kwenye mteremko mkali.
"Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia dereva wa gari aina ya Scania iliyokuwa imebeba shehena ya maji tani 30, ilisababisha ajali kwa kuigonga gari ya abiria aina ya  Noah kwa nyuma na kusababisha vifo vya watu watano na majeruhi wanne,"amesema RPC Maigwa.
Kamanda Maigwa amesema mpaka sasa mwili mmoja ndio uliotambulika wa Philipo Makaka (65) mkazi wa Arusha na miili minne bado haujatambuliwa ambayo ipo katika Hospitali ya Faraja, iliyopo mji mdogo wa Himo.
Aidha Kamanda Maigwa amewataja majeruhi hao kuwa ni Neema Shirima (23) mkazi wa Rombo, John Macha (22) mkazi wa Soweto Moshi, Natalia Assenga (43) mkazi wa Mengwe Rombo na Dismas Mrema (45) ambaye alikuwa ni dereva wa gari aina ya Noah.
Akizungumzia hali za majeruhi waliolazwa katika hospitali ya Faraja, Mganga Mfawidhi Msaidizi wa hospitali hiyo, Doreen Massawe amesema hali za majeruhi hao zinaendelea kuimarika ambapo pia ametoa wito kwa wananchi ambao hawajawaona ndugu zao tangu jana kufika kuitambua miili iliyohifadhiwa katika hositali hiyo.
"Majeruhi mmoja amehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC akiendelea na matibabu, mwingine ndugu waliomba wakamhudumie karibu na nyumbani. Hapa wapo majeruhi wawili ambao ni dereva wa Noah ambaye alipata michubuko kwenye mapafu na mkono wake, na mwingine nyonga ilisogea na tayari tumeirudisha na wote wanaendelea vizuri," amesema.