Dk Kihamia ateua kaimu mkurugenzi jiji la Arusha

Muktasari:

  • Miongoni mwa tuhuma zinazomkabili Dk Pima na wenzake wengine watano ni pamoja na ubadhirifu wa fedha za Serikali.

Dar es Salaam. Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dk Athumani Kihamia leo Mei 26, 2022 amemteua Hargeney Chitukuro kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha.

Chitukuro anakaimu nafasi hiyo baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumsimamisha kazi aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji hilo, Dk John Pima Mei 24, 2022 ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazomkabili yeye na watumishi wengine watano wa Jiji hilo.

Kabla ya Uteuzi huo, Chitukuro alikuwa Katibu Tawala Msaidizi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Idara ya Uchumi na Uzalishaji Mali.

  • Kaimu Mkurugenzi jiji la Arusha, Hargeney Chitukulo akisaini kitabu mara baada ya kukaimishwa nafasi hiyo baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji hilo dokta John Pima kusimamishwa kazi hivi karibuni.

Miongoni mwa tuhuma zinazomkabili Dk Mpima na wenzake ni pamoja na ubadhilifu wa fedha za Serikali.