Dk Kimei alia na riba kubwa za benki

Mbunge wa Vunjo Dk Charles Kimei

Muktasari:

Mbunge wa Vunjo, Dk Charles Kimei amesema Sera ya fedha Tanzania bado ina upungufu mkubwa kwa kuwa haiwajali watu wenye kipato cha chini.

Dodoma. Mbunge wa Vunjo Dk Charles Kimei amesema Sera ya fedha Tanzania bado ina upungufu mkubwa kwa kuwa haigusi watu wenye kipato cha chini.

 Dk Kimei ametoa kauli hiyo leo Novemba 4, 2021 wakati akichangia mapendekezo ya mwongozo wa maandalizi ya mpango wa Serikali wa 2022/23 uliowasilishwa jana bungeni na Waziri wa Fedha Dlk Mwigulu Nchemba ambapo wanakadiria bajeti ya mwaka ujao iwe zaidi ya Sh39 trilioni.
"Sera itakuwa nzuri ikiwagusa watu, lazima tuangalie suala ma riba za benki, kwa Sasa ni kubwa mno lazima turudi kwenye single digital (tarakimu moja) ndipo tutafaulu," amesema Dk Kimei.
Amesema kuwa uwepo wa riba kubwa imekuwa ni faida ya benki na wanahisani wake wanaotengeneza faida kubwa lakini kwa wananchi ni maumivu.
Mbunge huyo amesema riba ikishuka itasaidia wananchi wengi kukopa kwa wingi na kufanya taasisi za fedha kuwa rafiki na wafanyabiashara.
Kwa mujibu wa Dk Kimei, riba ya asilimia 15 ni mateso kwao na ilipaswa jambo hilo lipitiwe na kutazamwa upya ili kuishusha kwa kuwa duniani kote sera ya fedha ni riba so kingine.
Naye Mbunge wa Mbeya Vijijini Oran Njeza amesema Mpango wa Maendeleo hautawagusa wakulima hivyo unaweza usiwe na faida kwa kundi la chini.
Njeza amesema kama ungegusa wakulima basi ungeonekana kuwa na faida kubwa hasa kwa kundi la chini.